23.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

Mhubiri Ezekiel Odero kufanya uponyaji, maombezi Mwanza, RC, RPC wabariki

Na Mwandishi Wetu, Mwanza

MHUBIRI mashuhuri nchini Kenya, Ezekiel Odero anatarajia kufanya mkutano wa siku tano kuanzia Julai 24 hadi 28, mwaka huu katika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza na kutoa huduma ya uponyaji, maombezi na miujiza kwa maelfu ya watu kutoka sehemu mbalimbali watakaohudhuria.

Mkutano huo uliopewa jina la ‘Miujiza na Ishara’ utaongozwa na Pasta huyo wa kanisa la New Life Prayer & Church la Mombasa nchini Kenya, huku akifanya mamombi ya kuliombea taifa na viongozi wake, uponyaji, ukombozi  na maombezi, huku akishukuru mamlaka za Tanzania kwa kumfungulia milango.

Akizungumza baada ya kufika jijini Mwanza, kukagua uwanja wa CCM Kirumba, kukutana na Mkuu wa Mkoa huo, Said Mtanda na Kamanda wa Polisi, Wilbroad Mutafungwa, Pasta Odero alisema watumishi wa Mungu wanapaswa kufikisha ujumbe waliotumwa na Mungu na siyo vinginevyo.

“Mimi Mungu amenituma nihubiri injili sasa anayekuja kupokea ni kazi yake mwenyewe. Ni muhimu kama kiongozi wa dini kutoa ujumbe kwa viongozi katika njia ambayo inaleta heshima kwao kwa sababu siasa na injili haziambatani, tuhubiri injili tuwashauri wanasiasa na tuwaombee lakini sisi tusifanye siasa,”

“Kinachofanya niipende Tanzania ni umoja na Amani, msibadilishe umoja wenu na amani mliyonayo. Mlinde hiyo ni dhahabu kubwa sana ambayo mko nayo, hiyo roho na neema ibakie Tanzania milele kwa sababu Tanzania inaweza kubaki kama mji ambao Mungu ametenga kwa ajili ya kuokoa mataifa,” alisema Pasta Odero 

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda, amesema mkutano huo ni fursa chanya kwa wakazi wa Mwanza kwani mkoa huo wenye wakazi milioni 3.7 utanufaika kiuchumi, kijamii na utalii kwani wageni wengi kutoka ndani na nje ya nchi watakaofika watautangaza mkoa huo.

“Nchi yetu bila maombi haiwezi kwenda tunaamini katika maombi n sala, siku zote watumishi wa Mungu ni watu ambao tunawapa ushirikiano mkubwa. Sisi tunaheshimu kila mtu na mafuta yake (upako), kazi anayofanya mtumishi wa Mungu mimi nikilazimisha sitaiweza.

“Ujio wa pasta Ezekiel ni kutangaza mkoa wetu wa Mwanza kwa sababu ana watu wengi wanaomfuatilia na wanaopata huduma kwake, kwahiyo watu wengi watakaomfuatilia watajua mambo mbalimbali kuhusu mkoa wetu, na wananchi wa Jiji la Mwanza watajiongezea kipato kwa huduma watakazotoa,” alisema Mtanda

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa, alisema mkutano huo utahusisha watu wengi hivyo jeshi hilo limejiandaa kuhakikisha usalama kwa watu wote watakaohudhuria, huku akiwataka wakazi wa Mwanza kutoa ushirikiano na kuwa walinzi wa mani.

Baadhi ya wakazi wa jijini hapa, Revinson Revelian na Marry Edward, wamesema wanatarajia mambo makubwa kwenye mkutano huo ikiwemo huduma ya uponyaji na maombezi ili kuepukana na changamoto mbalimbali wanazokutana nazo ikiwemo ajali za barabarani na magonjwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles