24.8 C
Dar es Salaam
Friday, October 4, 2024

Contact us: [email protected]

MBARAWA AZIBEBESHA MZIGO KAMPUNI ZA SIMU

Na MWANDISHI WETU- GAIRO

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, ameyataka makampuni ya simu kuhakikisha mawasiliano ya simu yanapatikana wakati wote katika ubora unaotakiwa ili kuwawezesha wananchi kupata huduma inayowiana na thamani ya fedha wanayolipa.

Akikagua na kuzindua minara ya simu ya kampuni za TTCL, Vodacom, Halotel na Tigo katika Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro, Profesa Mbarawa alisema Serikali itaendelea kushirikiana na kampuni za simu kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) ili katika kipindi cha miaka mitatu ijayo sehemu zote za Tanzania ziwe zimefikiwa na huduma ya mawasiliano ya simu ya uhakika.

“Tumieni mawasiliano ya simu kufanya biashara, kuboresha huduma za jamii kama elimu na habari ili kukuza ustawi wa maisha yenu,” alisema Profesa Mbarawa.

Amewaonya wananchi kujiepusha na matumizi mabaya ya mitandao ya simu kwani ipo sheria kali inayodhibiti matumizi mabaya ya simu.

Alisema kuna umuhimu wa kampuni za simu kujenga minara maeneo mapya na kukarabati minara ya zamani ili kuwezesha mawasiliano kuwa katika ubora maeneo yote ya nchi.

Aliwataka wakazi wa vijiji vya Letugunya, Leshata na Chakwale, kutumia fursa ya upatikanaji wa mawasiliano kuongeza uzalishaji wa mazao na kuyauza kwa bei nzuri na hivyo kukuza uchumi wao.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote, Mhandisi Peter Ulanga, alisema wamejipanga kukamilisha miradi yote kwa wakati.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles