24.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

Mashindano ya gofu NCBA kufanyika Novemba

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

MASHINDANO ya wazi ya gofu ‘NCBA Tanzania Open 2023’ yanatarajia kufanyika Novemba 23-26, 2023 ambapo zaidi ya wachezaji 200 watachuana kwenye viwanja vya Kili Golf, mkoani Arusha.

Hayo yamezungumzwa na Mwenyekiti wa Chama cha Gofu Tanzania(TGU), Gilman Kasiga, mbele ya waandishi wa habari jana Oktoba 24, 2023, wakati wa kusaini mkataba wa udhamini wa michuano hiyo na benki ya NCBA, jijini Dar es Salaam.

Kasiga amesema mashindano hayo yatashirikisha wachezaji wa kulipwa na ridhaa kutoka nchi za Burundi, Rwanda, Uganda, Kenya, Ethiopia, Zimbabwe, Afrika Kusini wenyeji Tanzania.

“Shindano hili ni kati ya mashindano yanayofanyika kila mwaka lakini mwaka jana hatukufanya, tuna imani litakuwa kubwa na wachezaji watapa zawadi mbalimbali,” amesema.

Akizungumzia udhamini waliopata kutoka NCBA mwenyekiti huyo, amesema watashirikiana nao katika mashindano hayo pamoja na kukuza vipaji kuanzia ngazi ya chini ya watoto.

“Nia yetu ni kuanzisha ushirikiano na wadau kama hawa, tutashirikiana nao katika mashindano haya lakini wamejitolea kufanya kazi na sisi katika kuendeleza mchezo wa gofu kuanzia ngazi ya chini vijana,” ameeleza Kasiga.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NCBA, Claver Serumaga, amesema wanajivunia kuingia mkataba huo wa udhamini kwani inathibitisha kujitolea kwao kwenye mchezo huo hapa nchini na kufikia vipaji vya Afrika nzima.

Naye Mkuu wa Masoko wa Vodacom ambao ni miongoni mwa wadhamini wa mashindano hayo, Aileen Meena, amesema wanasapoti mchezo huo, lengo likiwa ni kukuza ushirikiano na klabu za gofu Tanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles