29.7 C
Dar es Salaam
Monday, September 16, 2024

Contact us: [email protected]

Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar afungua mashindano ya BAMATA

Makamu wa Pili wa Rais Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Hemedi Suleiman leo Septemba 6, 2024 amefungua mashindano ya Michezo  ya  Baraza la Michezo la Majeshi Tanzania (BAMATA), huku akiwataka wananchi kujitokeza kuunga mkono michezo hiyo.

Mashindano hayo yanashirikisha  majeshi yote ya Ulinzi na Usalama nchini  ambapo itafanyika kwenye  Uwanja  Jamhuri Mkoani Morogoro.

Aidha ametoa pongezi kwa BAMATA kwa maandalizi mazuri, akielezea  umuhimu wa michezo hiyo ikiwa ni pamoja na kupunguza hatari ya kupata maradhi yasiyo ambukiza, kuhamasisha vijana kuacha uhalifu.

Aliyataka majeshi kutumia michezo hiyo kutengeneza umoja na mshikamano huku akisisitiza ichezwe kwa weledi na itumike kama kipimo cha kupima nidhamu ya majeshi yote.

Majeshi yatakayoshiriki michezo hiyo ni pamoja na JWTZ, Polisi, Magereza, Zimamoto, Idara Maalumu za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na waalikwa ambao ni Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA).

Michezo itakayochezwa ni  soka kwa wanaume na Wanawake, mpira wa kikapu, Pete, Wavu, riadha na ulengaji shabaha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles