29.7 C
Dar es Salaam
Wednesday, August 17, 2022

Magufuli: Viongozi jengeni utaratibu wa kuandika vitabu

Anna Potinus

Rais Dk. John Magufuli amewataka viongozi wastaafu nchini kujenga utaratibu wa kuandika vitabu vinavyohusu maisha yao ili viwe chachu kwa vijana wanaotamani kuingia katika masuala ya uongozi.

Ametoakauli hiyo leo Jumanne Novemba 12, alipokuwa akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kitabu cha historia ya maisha ya Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa kilichopewa jina la ‘My life my purpose’ iliyofanyika Jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na viongozi wengine mbalimbali wakiwemo marais wastaafu, Ali Hassan Mwinyi, Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.

“Ninawahimiza viongozi wastaafu wengine kuiga mfano wa mzee Mkapa kwa kuandika vitabu ili uzoefu wao katika uongozi uwe chachu kwa vijana wetu wanaoinukia kwenye uongozi, nimefurahi kusikia kuwa mchato wa kukamilisha kitabu cha Mzee Mwinyi uko mbioni kukamilika na Mzee Kikwete pia anaendelea na uandishi wa kitabu chake.

“Uandishi wa vitabu usiishie kwa viongozi wastaafu wa nafasi za urais tu tunataka na viongozi wengine nitafurahi kusoma kitabu cha Mzee Warioba, Maalim Seif, Job Ndugai na wengine wengi kwani haya ni masuala muhimu katika historia na maendeleo yetu,” amesema Rais Magufuli.

Aidha amewahimiza Watanzania kukuza na kujenga utamaduni wa kujisome akisema vitabu havitakuwa na manufaa yoyote kama havitasomwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,905FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles