23.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 10, 2024

Contact us: [email protected]

Infinix yaongeza furaha kwa wateja wake Msimu huu wa Sikukuu

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Infinix inaendelea kutoa zawadi kwa wateja wake katika msimu huu sikukuu ya Christmass na Mwaka mpya ambapo wateja wanaendelea kufika kwa wingi katika maduka ya kampuni hiyo kwa ajili ya kununua zawadi za simu kwa wapendwa wao.

Kupitia mitandao ya kijamii kampuni hiyo walitupia picha na jumbe zenye kutuhabarisha kuhusu promosheni hiiyo kubwa ambapo mteja akifanya manunuzi katika maduka yao atakuwa umejiweka kwenye nafasi ya zawadi zenye thamani hadi ya Sh 3,000,000.

Kwa mujibu wa Afisa Uhusiano wa Infinix, Aisha Karupa alisema: “Tumefuraishwa na muitikio huu mkubwa wa wateja, huu ni mwezi wa kuzidisha upendo, tumeandaa zawadi nyingi kwa ajili ya wateja wetu pia tumefanya punguzo kubwa kwenye bidhaa zetu, chakufanya wewe mteja wetu nunua matoleo haya ya simu ‘Infinix HOT 40 Series, NOTE 30 series, HOT 30 series, Zero 30 Series katika duka lolote la simu lililopo karibu yako kwani hii ni ya wote wa Mikoani na wa Mkoa wa Dares Salaam,” amesema.

Zawadi nyingine zimetajwa kuwa ni Pikipiki, Laptop, vocha za manunuzi zenye thamani ya Sh 100,000 huku nyingine zikitolewa papo hapo.

Ameongeza kuwa hakuna haja ya kuwaza kuhusu zawadi na simu yenye feature za kisasa kwa umpendae wakati huu wa sikukuu kwani promosheni hiyo itaendelea kuwepo katika msimu wote huo.

Infinix HOT 40 pro, HOT 40i, NOTE 30, HOT 30 na Zero 30 ni matoleo ambayo yamefanya vizuri na yanaendelea kufanya vizuri katika mauzo.

Note 30 vip iliweza kuipaisha infinix kutokana na teknolojia ya fast chaji ambapo hadi sasa inatambulika kuwa simu pekee yenye teknolojia hiyo yenye bei nafuu sokoni. Infinix NOTE 30 Vip ina Watt 68 ya chaji ya haraka na Watt 50 ya wireless chaji.

Infinix HOT 40pro na HOT 40i zimezinduliwa rasmi kwenye soko la simu nchini sambamba na mashindano ya game za simu wikiendi hii Hot 40pro imenadiwa vikali na Director Nikolasi mtengenezaji wa video za music kutokana ubora wa processor wa simu hiyo pamoja na unafuu wa bei wa simu hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles