25.1 C
Dar es Salaam
Thursday, May 2, 2024

Contact us: [email protected]

ICRC yakabidhi baiskeli TWBA

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Taasisi ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC), imekabidhi baiskeli mwendo 12 ‘wheelchairs’ kwa timu ya mpira wa kikapu cha watu wenye za ulemavu ‘wheelchair basketball’.

Baiskeli hizo zinazotumika kuchezea  mchezo huo, vimekabidhiwa leo Novemba 23, 2023   mbele Katibu Mtendaji Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Neema Msitha jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa makabidhiano  hayo, Neema Msitha amevitaka vyama vya michezo nchini  kuwa wabunifu ili kushawishi wadau  kushiriki katika jithada za kukuza michezo nchini.

“Niwapongeze Chama Cha Mchezo wa Kikapu cha Watu wenye za ulemavu Tanzania kwa kuendelea kukuza mchezo huu kwa kuhusisha wadau mbalimbali. Nitoe rai kwa vyama vingine vya michezo kuwa wabunifu na kujipambanua ili kuwashawishi wadau,” amesema Neema.

Naye  Katibu wa Chama Cha Mchezo wa Kikapu cha Watu wenye za ulemavu Tanzania (TWBA), Abdallah Mpogole, ameishukuru ICRC kutokana na mchango wao wa kuwasadidia vifaa vya mchezo huo mara kwa mara.

 “Tunaishukuru ICRC kwa msaada huu ambao sio mara ya kwanza, mara nyingine tuliweza kupeleka, mikoa ya Kilimanjaro, Iringa na Zanzibar, na nia yetu ni kufika mikoa yote ili mchezo huu, uchezwe kila pande ya nchi,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles