24.6 C
Dar es Salaam
Monday, October 14, 2024

Contact us: [email protected]

EVERTON WAMKATA ROONEY MIL 900/-

LONDON, ENGLAND

HATIMAYE uongozi wa klabu ya Everton ya nchini Uingereza, imetangaza kumkata mshahara wa wiki mbili mshambuliaji wake, Wayne Rooney kutokana na kosa la kuendesha gari akiwa amelewa.

Kwa sasa Rooney ndani ya klabu hiyo anachukua kitita cha pauni 150,000 kwa wiki ambazo ni zaidi ya milioni 451, hivyo mishahara ya wiki mbili ni sawa na pauni 300,000 ambazo ni zaidi ya milioni 902 za Kitanzania.

Everton wameweka wazi kuwa fedha hizo ambazo Rooney atakatwa zitapelekwa moja kwa moja kwa watu wasiojiweza kwa kuwa klabu hiyo ina mradi wa kusaidia watu wenye uhitaji maalumu, hivyo wanaamini fedha za Rooney zitasaidia sana kwa watu hao.

Rooney mwenye umri wa miaka 31, aliomba kusamehewa na klabu hiyo ili aepuke adhabu hiyo, lakini klabu imefanya maamuzi hayo ili kuwa sehemu ya fundisho kwa wengine.

Mapema wiki hii Rooney alihukumiwa kutoendesha gari kwa miaka miwili baada ya kukamatwa Septemba mosi, akiwa anaendesha gari huku amelewa. Mbali na kuhukumiwa kifungo cha kutoendesha gari kwa miaka miwili, pia anatakiwa kufanya kazi za kijamii kwa jumla ya saa 100 ndani ya miezi 12.

Hata hivyo, mke wa mchezaji huyo Coleen Rooney ameonekana kufurahia kitendo cha mume wake kupewa adhabu hiyo na kukatwa kwa mshahara kwa kuwa anaamini itakuwa funzo kwa baba wa watoto wake.

“Kuna wakati Rooney anafanya mambo kama mtoto, naweza kusema nina watoto wanne sasa kwenye nyumba yetu akiwa pamoja na Rooney, naweza kusema kuwa huu ni wakati wa Rooney kuwa mwanamume,” alisema Coleen.

Rooney wakati anakipiga katika kikosi cha Manchester United msimu uliopita kabla ya kujiunga na klabu ya Everton, alikuwa anachukua kiasi cha pauni 300,000 kwa wiki, lakini baada ya kujiunga na Everton anachukua nusu ya fedha hizo.

Kabla ya kuondoka kwake Manchester United, kulikuwa kunamfanya awe mchezaji anayelipwa fedha nyingi katika Ligi Kuu ya nchini England hadi kufikia majira ya joto, huku akifuatiwa na kiungo mshambuliaji wa Man United, Paul Pogba ambaye anachukua kiasi cha pauni 290,000 kwa wiki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles