32.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 1, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Nchimbi awakosha wananchi Mbarali, akitoa maelekezo kutatua kero zao

Na Mwandishi Wetu, Mbarali

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi, amewakosha wananchi wa Mbarali, alivyowaruhusu wawasilishe kero zao kwa njia ya maswali na yeye kuyajibu papo kwa papo kwenye mkutano wa hadhara, na kutoa maelekezo kwa viongozi na watendaji wa chama na Serikali, kwa ajili ya hatua mbalimbali za kutatua na kuzimaliza.

Kuhusu utatuzi wa mgogoro wa mpaka kati ya Hifadhi ya Ruaha, ambayo iko chini ya TANAPA, Balozi Nchimbi ameelekeza Wizara ya Ardhi, kuhakikisha wataalam wa upimaji ardhi wanafika Mbarali mara moja kujiridhisha juu ya migogoro ya mipaka kwa wananchi dhidi ya taasisi za kiserikali.

Akizungumza katika mkutano huo wa hadhara baada ya kusimama kuwasalimia wananchi wa Mbarali, katika Kata ya Ubaruku, pia amemuelekeza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera na Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, kwa pamoja, kuhakikisha wanasimamia na kufuatalia juu ya tuhuma za baadhi askari wa TANAPA kutumia nguvu zinazoumiza na kutweza utu wa binadamu.

Amewataka kuhakikisa matukio ya ukatili yanapingwa, kukemewa na kukomeshwa, baada ya kupokea kero zilizodai na kuwatuhumu baadhi ya askari wa TANAPA wanawapiga risasi wananchi, hasa vijana wanaokwenda kuvua samaki kukatiza kwenye maeneo yasiyo njia rasmi.

Aidha, Balozi Nchimbi alimuagiza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kusimamia na kuhakikisha watu wanapewa elimu ya kutosha na kuoneshwa maeneo sahihi ya njia za kupita wakati wakienda kwenye shughuli zao za kujipatia kipato na kuendesha maisha yao.

Kuhusu kero iliyodai kuwapo kwa vitendo vya kuwatoza wakulima kwa mazao yaliyoko shambani, amemuelekeza Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mbarali kuishughulikia na kuimaliza ili wananchi wasihangaishwe.

Balozi Nchimbi amuelekeza Waziri wa Kilimo Hussein Bashe, kuanza mazungumzo mara moja na Haroun Mulla ambaye ni mmoja wa wawekezaji wakubwa wa sekta ya kilimo katika eneo hilo, akimiliki Kampuni ya Mbarali Estates, aliyekubali kujadiliana kwa ajili ya kuachia shamba moja kwa matumizi ya wananchi wapate mahali pa kulima.

Aidha, Balozi Nchimbi alitumia fursa hiyo kuwasilisha salamu za upendo za Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa wananchi wa kata ya Ubaruku, Wilayani Mbarali Mkoa wa Mbeya walipakana na hifadhi ya Taifa ya Ruaha.

” Rais Dk Samia yupo nchini Uturuki kikazi lakani amenipa salamu zake niwapatie wananchi wa hapa Ubaraku, anatambua thamani yenu na anawataka kuendelea kuwa na imani na mbunge wenu na CCM kwa ujumla wake .”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles