25.1 C
Dar es Salaam
Thursday, May 2, 2024

Contact us: [email protected]

DC Ukerewe akagua mapokezi wanafunzi kidato cha tano

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, Hassan Bomboko ametembelea na kukagua shule tatu za Sekondari ambazo zipo kwenye mapokezi ya wanafunzi wa kidato cha tano huku akiwataka wazazi na walezi ambao watoto wao hawajaripoti kuwawahisha shuleni ili kuondoa tofauti ya uelewa wa ujifunzaji darasani.

Akizungumza kwa nyakati tofauti kwenye shule hizo Agosti 18, 2023 ambazo ni Bukongo, Pius Msekwa na Ukerewe Sekondari Bomboko amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan imeboresha na kutekeleza ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya elimu wilayani humo lengo likiwa ni kuhakikisha  maeneo rafiki ya ufundishaji na ujifunzaji.

“Lengo la ziara yangu ni  kutaka  kujionea zoezi la kupokea wanafunzi wa Kidato cha tano 2023 linavyoendelea ndani ya wilaya yetu, nitoe wito kwa wazazi na walezi ambao watoto wao wamechaguliwa kujiunga na shule za sekondari zilizopo wilayani humu kwa masomo ya kidato cha tano wahakikishe wanawahi kuwapeleka shuleni ili waanze masomo maana wenzao waliowahi kuripoti wameishaanza.

“Miundombinu ya elimu ni mizuri kabisa, vijana hao ndiyo  hazina ya taifa letu la kesho  kwa kutambua hilo serikali  imeboresha miundombinu katika sekta ya elimu hivyo ni wajibu wa wazazi na walezi kuhakikisha hakuna mwanafunzi anayekosa fursa ya kusoma ama kuchelewa kuanza masomo,” amesisitiza Bomboko.

Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa Wilaya ya Ukerewe Shule ya Sekondari Ukerewe inauwezo wa kupokea wanafunzi 500 wa bweni, ilipangiwa jumla ya wanafunzi 484 hadi Agosti 18 mwaka huu wanafunzi walioripori ni 120.

Amefafanua kwamba   Shule ya Sekondari Bukongo  wanafunzi  waliokwisharipoti ni 80 kati ya 249   waliopangiwa na serikali kujiunga na shule hiyo kwa mwaka wa masomo 2023/2024  yenye uwezo wa kupokea wanafunzi 250.

“Katika Shule ya Sekondari Pius Msekwa jumla ya Wanafunzi  70 kati ya 107 waliopangiwa na Serikali kujiunga kwenye shule hiyo yenye uwezo wa kupokea wanafunzi 150 ndiyo waliokwisharipoti ni matumaini yangu kwamba hadi Agosti 23, 2023 wanafunzi wote watakuwa wamekwisharipoti ili wasipitwe na masomo,” amesema Bomboko na kuongeza:

“Nimekagua shule zote za advance zilizopo katika Wilaya yangu ya Ukerewe ikiwepo Bukongo, Pius Msekwa na Ukerewe, nimejiridhisha, miundombinu ipo safi, kila shule ina mabweni ya kutosha kuwalaza wanafunzi wetu watakaofika kuanza masomo mwaka huu, madarasa yapo ya kutosha mazuri na ya Kisasa, viti na meza zipo za kutosha, vitanda vipo, walimu wa kombi zote kwa kila shule wapo na tayari wameanza kutekeleza wajibu wao wa kufundisha.

“Ninawasisitiza Wazazi wote walio na wanafunzi ambao wamepangiwa katika Wilaya yangu wafike kuanza masomo yao haraka ili kuondoa utofauti wa uelewa katika ufundishaji na ujifunzaji darasani, sisi hatusubili, masomo yameshaanza na kila kitu kipo sawa kuhakikisha wanafunzi wanapokelewa na wanapata huduma zote za msingi ikiwepo lishe,” amesema.

Kwa upande wake Kaimu Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Ukerewe, Mwalimu Evarista Msule amesema uboreshaji wa miundombinu ya elimu wilayani humo kumewezesha walimu kufundisha na wanafunzi kujifunza kwa ufasaha hivyo kuongeza ufaulu.

“Matokeo ya kidato cha sita mwaka 2023 shule ya sekondari Bukongo wanafunzi 41 walipata daraja la kwanza, 84 daraja la pili, 35 daraja la tatu na mwanafunzi mmoja tu ndiye alipata daraja la nne, hakuna aliyepata sifuri.

“Pius Msekwa sekondari wanafunzi 58 walipata daraja la kwanza, 18 daraja la pili, saba walipata daraja la tatu hakuna aliyepata daraja la nne na sifuri, kwa upande wa Ukerewe Sekondari bado hawajahitimu kidato cha sita na tunatarajia awamu ya kwanza watahitimu mwaka 2024, ni ukweli usiopingika kwamba mafanikio haya yametokana na mazingira bora ya kujifunza na kufundishia,”amesema Msule.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles