28.4 C
Dar es Salaam
Sunday, May 12, 2024

Contact us: [email protected]

DC Jokate ahimiza wananchi kutumia Uzazi wa Mpango

Na Jeremia Ernest, Mtanzania Digital

MKUU wa Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam, Jokate Mwegelo amesisitiza wananchi kutumia uzazi wa mpango katika kujenga familia zao.

Mwegelo ametoa wito huo leo Jumatatu Septemba 26, 2022 katika Madhimisho ya siku ya Uzazi wa Mpango Duniani yaliyofanyika katika Hospitali ya Mbagala Rangi tatu, jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo.

Hafla hiyo iliyo andaliwa na Shirika la DKT Internatiol Tanzania, ambapo limezindua kampeni ya Jipange kupitia ni vidonge vya uzazi wa mpango vya Trust Liliy vya muda mrefu, Trust Daisy vya muda mfupi, Kitanzi na Fiesta Condomu na Bull Condomu.

Akizungumza na wananchi katika uzinduzi huo Jokate amewaambia kuwa familia bora ni lazima iwe na mikakati mizuri wakianzia kujipanga katika swala zima la uzazi.

“Familia zetu tunatakiwa kujipanga katika swala zima la uzazi kwani litasaidia katika maendeo yetu na ya taifa kwa kuwa tukifanikiwa kupata watoto kwa mpango itatusaidia katika malezi bora ambayo itatusaidia kupunguza ‘Panya Road’ na watoto wa mitaani,” amesema Mwegelo.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa wilaya ametembelea Wodi za mama waliotoka kujifungua na kuwapatia zawadi kutoka DKT Internationl Tanzania, huku akiipongeza kampuni hiyo kwa kuamua kuanzia katika wilaya ya Temeke kutoa elimu ya uzazi wa mpango kwa kufundisha njia sahihi za kutumia pamoja na wauguzi wa hospitali hiyo kwa kazi kubwa wanayofanya.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Uzazi wa Mpango katika hospitali ya Mbagala, Elizabeth Bita, ameeleza kuwa kwa mwezi ofisi yake inapokea watu zaidi ya 700 wanaofata uzazi wa mpango na wengi wao hupenda njia ya kitanzi cha miaka mitatu kwa kuwa ni kirahisi.

Nae, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Irene Haule amewaomba kampuni ya DKT Internationl Tanzania, kutembelea shuleni kutoa elimu ya uzazi wa mpango kwa kuwa wanafunzi wengi wanakatisha masomo kwa sababu ya kupata mimba zisizotarajiwa.

“Wanafunzi wengi wanaogopa kutafuta njia za kujikinga na mimba kutokana na mazingira yao wanatumia dawa za p2, tofauti na matumizi yake, niwaombe DKT Internationl Tanzania kuwatembelea na kutoa elimu ya matumizi jinsi ya kujikinga na mimba,” amesema Dk.Haule.

Kwa upande wa mwakilishi wa Dkt Tanzania, Deogratius Kitama, alishukuru mkuu wa wilaya kwa kuungana nao katika uzinduzi wa kampeni ya Jipange na kuahidi kutoa ushirikiano pale watakapo hitajika katika upande wa uzazi wa mpango ili kutengeneza jamii bora.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles