Chynna Rogers afariki dunia

0
1480

PHILADELPHIA, MAREKANI

RAPA ambaye pia ni mwanamitindo Chynna Rogers, amefariki dunia huku akiwa na umri wa miaka 25, baada ya kuugua ghafla.

Meneja wa msanii huyo pamoja na familia yake imethibitisha kifo hicho, lakini hada sasa hawajaweka wazi chanzo chake.

“Hii ni siku ambayo siwezi kuisahau, itakuwa ngumu lakini hakuna namna, ukweli ni kwamba Chynna amepoteza maisha, Chynna tulimpenda na tutaendelea kumpenda katika maisha yetu,” alisema Meneja wa msanii huyo.

Mrembo huyo kabla ya kuanza kufanya muziki, alitokea kwenye mitindo, alianza kufanya kazi hiyo akiwa na umri wa miaka 14, alianza kufanya muziki baada ya kuwa rafiki wa karibu na A$AP Yams na A$AP Mob. Wimbo wake wa kwanza ulijulikana kwa jina la Selfie, ambao aliuachia mwaka 2014 pamoja na wimbo mwingine wa Glen Coco.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here