24.2 C
Dar es Salaam
Monday, May 13, 2024

Contact us: [email protected]

CCM Z’bar yatoa pole ajali ya kivuko Ukerewe


NA IS-HAKA OMAR-ZANZIBAR

Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Taifa Zanzibar, imetoa salamu za rambi rambi kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dk. John Magufuli kutokana na ajali ya Kivuko cha MV Nyerere ambayo imesababisha vifo vya zaidi ya watu 100 katika Kisiwa cha Ukara, wilayani Ukerewe.

Akitoa salamu hizo jana katika kikao cha kamati hiyo mjini Unguja Makamu Mwenyekiti wa CCM, Dk.Ali Mohamed Shein ambaye ni Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, alisema kamati hiyo imesikitishwa na ajali hiyo iliyotokea Septemba 20 mwaka huu mkoani Mwanza.

Alisema taarifa ya ajali ambayo imesababisha vifo vya watu wengi imewasikitisha wanaCCM kwa upande wa Zanzibar na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar(SMZ) na kwamba Zanzibar iko pamoja katika kuomboleza msiba huo mkubwa wa taifa.

“Taarifa iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Dk. John Magufuli ya uamuzi wa Serikali kuomboleza siku nne na bendera kupepea nusu mlingoti ni dhahiri kuwa ni msiba mkubwa kwa Tanzania.

“Sisi kwa upande wa Zanzibar tulikuwa na sherehe mbili kubwa tumeziaharisha zote kwa kuwa tunaomboleza kwa maagizo ya Rais Dk.Magufuli,” alisema Dk.Shein.

Rais Dk.Shein alisema ilitarajiwa kufanywa sherehe kubwa za kuwatunuku zawadi wanafunzi wa kidato cha sita waliofaulu lakini shughuli hizo zimeaharishwa kutokana na ukubwa wa jambo hilo.

Dk. Shein aliongeza kuwa sherehe zote zilizotakiwa kufanyika visiwani humu zimeharishwa kutokana na kuwepo kwa msiba huo mkubwa na kwamba Zanzibar inaungana na ndugu na jamaa katika kuomboleza.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa CCM,Zanzibar Dk. Abdulla Saadalla Juma  alisema kamati hiyo maalum imetoa Sh milioni tano kwa ajili ya mchango wa rambirambi wa msiba huo na kwamba kiasi hicho ni cha kuanzia.

Alisema CCM kwa upande wa Zanzibar ina ungana na wafiwa wote wa msiba huo na kwamba chama kitaendelea kutoa mchango wake kadri mahitaji yatakapohitaji

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles