31.2 C
Dar es Salaam
Monday, May 13, 2024

Contact us: [email protected]

Bilioni 2.5 zatumika kununulia mtambo wa kufundishia DMI

Na Mwandishi Wetu

Serikali kupitia Wizara ya Uchukuzi imetumia zaidi ya sh. 2.5 bilioni (2,744,106,712.35)  kununulia mtambo wa kisasa wa kufundishia katika  Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI)

Mkuu wa chuo hicho, Dk.Tumaini Gurumo amesema mtambo huo (Crane Simulator) utasaidia kufundishia wanafunzi kwa vitendo na kuongeza thamani ya elimu inayotolewa katika chuo hicho pekee hapa nchini.

“Mtambo huu unasiadia kufundishia katika kozi ambazo utendaji kazi wake ni maeneo ya bandari, viwandani na migodini. Zaidi ya shilingi bilioni mbili nukta tano zimetumika kununulia mtambo huu mpaka kufungwa hapa chuoni,” amesema Dk.Tumaini.

Mwanafunzi wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam akiwa kwenye mtambo (Crane Simulator) wa akifanya mazoezi ya kuendesha mtambo huo mpya ambao umenunuliwa kwa zaidi ya shilingi 2.5.

Kwa upande wake mtaalamu wa mtambo huo, Elinathan Blasius,  ambaye ni mkufunzi wa chuo hicho,  mtambo ni muhimu kwa wanafunzi kwani utasaidia kupata elimu ya kuendesha mitambo mabalimbali.

“Mtambo huu una mada zaidi ya kumi hivyo kila mwanafunzi atapata elimu ambayo itamsaidia kuendesha mitambo mikubwa na midogo,” amesema Elinathan.

Naye mwalimu Leonard Mwesiga amesema kuwa mtambo huo ni muhimu sana kwa chuo hicho kwani unaweza kufundishia zaidi ya masomo sita na mwanafunzi akihitimu katika masomo hayo ataweza kuendesha mitambo ya aina yoyote  katika sekta ya bandari,viwandani na migodini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles