25.1 C
Dar es Salaam
Thursday, May 2, 2024

Contact us: [email protected]

BETIKA haipoi Kariakoo Derby, Washindi 56 kuishuhudia kesho kwa Mkapa

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

WASHINDI 56 Promosheni ya Mtoko wa Kibingwa msimu wa 07 kuitazama Derby ya Kariakoo kati ya Yanga na Simba itakayofanyika kesho kwenye uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Wanahabari mapema leo Aprili 19, 2024 Afisa Habari wa Kampuni ya Betika Tanzania, Juvenalius Rugambwa wakati akiwapokea Washindi Promosheni ya Mtoko wa Kibingwa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julias Nyerere amesema washindi hao wamepatikana kupitia droo ya mtoko Kibingwa iliyoanza Mapema Februari 2024.

“Kama mnavyowaona hawa ni washindi ambao wamepatikana kupitia kampeni yetu ya mtoko kibingwa na hawa washindi waliowasili leo wataenda kuungana na wenzao wa Dar es Salaam nakukamilisha idadi kamili ya washindi 56 na wote watakwenda kulala kwenye hoteli yenye hadhi ya nyota tano wakifatiwa na bata la Mbagala zakiem kushuhudia burudani ya Muziki wa Bongofleva itakayodondoshwa na chino Wana Man, Mczo, Platform, sholo Mwamba na wengine kibao,” amesema Rugamwa.

Rugambwa ameongeza kuwa msimu huu wa mtoko wa kibingwa umekuwa wa kipekee zaidi kwani promosheni yote kulikua na ongezeko la zawadi kwa wki pamoja na mwezi ambapo wametoa zawadi za simu aina ya smartphone pamoja na Android kwa washindi mbalimbali mbali na zawadi kubwa ya kushinda tiketi ya kushuhudia derby yenyewe.

Pia amesema washindi watapelekwa na Ving’ora kwenye kuitazama Deby ya Yanga na Simba na watakaa jukwaa la watu maalum (VIP).

Hata hivyo, Jevenalius amesema kampuni ya Betika imekuwa ikitoa ushindi hapo hapo pia itaendelea kuonesha nia yao ya dhati kunyanyua michezo kuanzia mpira wa soko hadi kutoa udhamini katika michezo mbalimbali.

“Kama ambavyo tulivyo sisi mshindi akishinda anapewa zawadi zake hapohapo kwa haraka,tunawaomba watu waendelee kutupia ubashiri kwa kutembelea kwenye website yetu hata hii mechi ya Simba na Yanga ipo hapo,” amesema.

Kwa upande wake Balozi wa kampeni ya Mtoko wa Kibingwa, Baraka Mpenja amesema hii ni miongoni mwa derby inayowakutanisha watu kutoka Mataifa mbalimbali hivyo kwa washindi hao wanaenda kuandika historia mpya katika maisha yao na ndio dhamira ya Kampuni ya Betika kuhakikisha inawapa nafasi wateja wake .

Aidha amesema anawatakia mchezo mzuri timu zote mbili huku akiwapa moyo washindi hao kuwa watashuhudia mechi hiyo Kifahari zaidi (VIP).

Nao baadhi ya washindi hao akiwemo, Musa John kutoka Mkoa wa Tabora akiwa shabiki wa Simba ameishukuru kampuni ya Betika kupata fursa ya kuitazama Deby ya Kariakoo kwani ilikuwa ndoto yake kuona wachezaji wa timu hiyo.

“Kweli Betika hawana longolongo kwa mara ya kwanza nimepanda ndege hata nilipoambiwa nimeshinda sikuamini nilikua Shambani lakini baada ya siku kadhaa kunitafuta kwa mara ya pili na kunijulisha niwatumie vielelezo vyangu ili wanifanyie utaratibu wa safari ya kuja Dar es Salaam niliamini hivyo nawashukuru sana Betika,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles