26.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

Bashungwa awashukia wakandarasi Tanga

Na Mwandishi wetu, Tanga

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amemtaka Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS),  Mhandisi Mohammed Besta,  kukamilisha usanifu wa barabara ya Mkata- Kwamsisi ya kilomita 36, ifikakapo  Disemba 31, 2023.

  Akizungumza katika ziara yake ya kukagua athari za mvua za vuli  mkoani humo leo Novemba 24, 2023, Bashungwa amesema fedha za mradi huo zipo tayari hivyo kinachotakiwa ni kazi ya usanifu ifanyike haraka ili ujenzi uanze mara moja.

“Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ameashatoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara hii, hivyo kazi ya usanifu ikikamilika ujenzi uanze haraka,” amesisitiza  Bashungwa.

Amezungumzia umuhimu wa watendaji wa TANROADS wa ngazi zote kushirikiana na mamlaka za serikali ya mitaa ili kurahisisha ufuatiliaji wa kazi za wakandarasi na kuwezesha kufutilia haki za watumishi katika miradi ya ujenzi.

 Naye Mtendaji Mkuu wa TANROADS,  Mhandisi Besta amesema  wamejipanga kuhakikisha usanifu unakamilika kwa wakati na taratibu za kumpata mkandarasi wa ujenzi huo unakamilika mapema iwezekanavyo.

Katika hatua nyingine Waziri Bashungwa amemuonya vikali mkandarasi wa  kampuni ya kutoka China anaejenga  barabara ya Mkange-Tungamaa-Pangani yenye urefu wa kilomita 120.8 kuhakikisha anaongeza kasi  kwani serikali haitavumilia utetezi wowote unaochelewesha.

“Gharama za ucheleweshwaji wa ujenzi wa barabara serikali haitavumilia mkandarasi yoyote atakayechelewesha mradi.

“TANROADS endelea kuwahimiza  wakandarasi na wasimamizi wa miradi ambao hawakamilishi kazi kwa wakati wasipewe kazi nyingine,”amesema Bashugwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles