26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, August 14, 2022

BARR KUWASILISHA RIPOTI YA MUELLER

Mwanasheria mkuu wa Marekani William Barr atafika bungeni kwa mara ya pili wiki hii wakati wabunge, ikulu ya White House na umma nchini Marekani ukisubiri kwa hamu kuwasilishwa kwa ripoti ya mchunguzi maalum Robert Mueller kuhusu Urusi ilivyohusika katika uchaguzi nchini Marekani.

Barr atazungumza katika kamati ndogo ya kupanga matumizi leo, ikiwa ni tukio la pili la siku mbili la kikao juu ya bajeti ya idara yake.

Kama wabunge walivyokuwa jana, maseneta wanatarajiwa kujihusisha zaidi na karibu kurasa 400 za waraka huo kuliko maelezo ya bajeti.

Barr amewaambia wabunge kuwa anatarajia kuwasilisha sehemu ya ripoti hiyo wiki hii. Maafisa wa wizara ya sheria wanaiangalia ripoti hiyo na kuondoa taarifa zilizoko mahakamani na maelezo yanayohusiana na uchunguzi ambao bado unaendelea, miongoni mwa vipengee vingine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,656FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles