26.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 3, 2022

Andy Crossman atua Zikomo Awards

Lusaka, Zambia

Kuelekea tuzo za Zikomo Africa Awards zitakazofanyia jijini Lusaka, Zambia Oktoba 15, 2022, Andy Crossman anatarajiwa kupewa tuzo ya heshima.

Andy ambaye ni Mwanasaikolojia, Mjasiriamali na Mfadhili wa Kibinadamu anayeendesha kampuni zinazosaidia watu walio katika mazingira magumu, wenye ulemavu kujitegemea na kuwapa heshima katika jamii zao.

Mapenzi yake hayo kwa wahitaji yamefanya atambuliwe na Jumuiya ya Waafrika huko Idaho, Marekani na kwingineko kwani ametoa ajira na fursa nyingi kwa wakimbizi.

Chanzo cha ndani kutoka kwenye tuzo hizo kimeweka wazi kuwa Andy ni mfanyakazi wa kujitolea katika Kamati ya Kimataifa ya Uokoaji ambapo anasaidia na ustadi wa makazi mapya na ajira kwa wakimbizi waliofika hivi karibuni nchini Marekani.

Aidha, Andy na mkewe Lindsey ni wafadhili wanaofanya kazi kwa NGOs zinazotoa usaidizi barani Afrika kama vile Kiva, Because International, Ghana Make a Difference, WaterAid na Charity:Water.

“Andy anajulikana kwa kusaidia ustawi wa Waafrika huko Idaho hasa katika kujifunza Kiingereza na ujuzi wa kompyuta, kufanya kazi kuelekea uraia, na kuhakikisha kwamba familia zao ziko imara na zinatunzwa.

“Tunayo furaha kutangaza kwamba Andy ameteuliwa na Zikomo Awards kwenye kipengele cha Utu ambapo inamfanya Andy kuwa mtu wa kwanza kuteuliwa kutoka nje ya Afrika, tuzo zitatolewa Bonanza Resort hapa Lusaka,” kilisema chanzo hicho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,573FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles