33.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Wananchi tumieni kilimo cha mkakati- Dk. Mpango

Mwandishi Wetu – Kigoma

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Isdor Mpango, amewataka wakazi wa mkoawa Kigoma kujishughulisha na kilimo cha mazao ya kimkakati na kutumia vema soko linalopatikana ndani ya nchi pamoja na nchi jirani ya Burundi kujipatia kipato ili kuondokana na umasikini.

Dk. Mpango ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Buhigwe mkoani Kigoma, alitoa rai hiyo alipotembelea kata za Kilelema, Muyama na Kasumo wilayani Buhigwe kuhamasisha shughuli za maendeleo na kuwashukuru wananchi kwa kumchagua Dk. John Magufuli, kuwa Rais wa Tanzania na yeye binafsi kuwa mbunge.

Alwashauri wananchi hao kujihusisha na kilimo cha mazao ya kimkakati ikiwemo kilimo cha parachichi, mawese, tangawizi, kilimo cha mbogamboga na matunda na kwamba Serikali kwa upande wake itapeleka mbegu za kisasa ili kuwa na uzalishaji wa mazao wenye tija.

Aliwahimiza kuhakikisha wanalinda amani, usalama na utulivu wa nchi kwa nguvu zote ili wananchi waendelee kujiletea maendeleo yao katika nyanja mbalimbali za kiuchumi katika mazingira ya amani na utulivu.

Aliwaahidi wananchi wa kata hizo, ahadi zote alizo ahidi wakati wa kampeni kwenye sekta ya elimu, maji, afya, nishati, ujenzi wa miundombinu ya barabara pamoja na kuendeleza kilimo, zitatekelezwa kwa awamu katika kipindi cha miaka 5 ijayo.

Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Kanali Michael Ngayalina, alimwomba Dk.Mpango kusaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili wilaya yake kwa upande wa maji, barabara, soko la kimataifa pamoja na suala la elimu.

Kanali Ngayalina alieleza mikakati mbalimbali iliyopo ya kukabiliana na changamoto ya maji, Serikali inatekeleza mradi wa maji wenye thamani ya Sh bilioni 2.8 utakao pita katika vijiji vya Migongo na Kilelema pamoja na ujenzi wa daraja la Mto Malagarasi litakaloiunganisha wilaya yake na nchi jirani ya Burundi, ikiwa ni sehemu ya mradi wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Kabingo mpaka Manyovu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles