25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Tanga Cement yasema imejipanga kutoa huduma bora

Mwandishi Wetu- Dar es Salaam

UONGOZI wa kiwanda cha  Tanga Cement, umesema uko tayari kuendelea kuboresha bidhaa zake ili kuuunga mkono jitihada kubwa zinazofanywa na Rais Dk. John Magufuli ili kufikia uchumi wa viwanda.

Umesema pamoja na kukabiliwa na mazingira ya changamoto mbalimbali katika sekta hiyo, umejipanga vizuri kuhakikisha unatoa huduma bora kama ambavyo umekuwa ukifanya miaka yote.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam mwishoni mwa wiki Dar es Salaam,  wakati wa kuwasilisha tarifa za biashara za kampuni hiyo kwa mwaka unaoishi Desemba 31,mwaka jana, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kiwanda hicho, Wakili Lawrance Masha alisema wamejipanda vizuri ili kuhakikisha wanaongeza uzalishaji wa saruji bora na kusambazwa maeneo yote ndani na nje nchini.

Alisema  kampuni itaendelea kuwalinda kufanyakazi na wakandarasi ili kuhakikisha wanendelea kuona fahari ya kazi wanayoifanya ili kukidhi ongezeko na ukuaji wa mahitahji katiuka sekta ta ujenzi ya Tanzania.

“Pamoja na kuwepo kwa changamoto, mfumuko wa beki uli[ungua kwa mwaka na kufika silimia 3.4 mwak mwaka 2019 kutoka asilimia 3.5 mwaka 2018 ambao ulisababishwa na matokeo ya sera za hazina za kifedha za Serikali,’ alisema.

Alisema utendaji wa kiuchumi ulibali kuwa thabiti kukiwa na ukuaji wa patio la taifa las ilimi 6.8 kwa mwaka 2019 ikilinganishwa na asilimia 7.1 kwa mwaka 2018.

“Kampuni ina matumaini chanya yanayotokana na mipango ya maendeleo ya miundombinu chini ya progamu ya maendeleo ya Serikali ya mwaka 2025 ambapo tunatarajia miradi mingui kuendelea kushika kasi ndani ya mwaka 2020.

“Kampuni ina imani na hatua zilizochukuliwa na Serikali kudhibiri uchumi kutokana na uwekezaji wa athari ambazo zingeweza kusahabishwa na ugonjwa wa hpma kali ya mapafu (Covidi-19) na kuahidi kigamnyakazio pamoja na Serikali katika kukuza uchumi.

Alisema kampuni hiyo imeahidi kukidhi mahitahji ya saruji nchini kwa kiwango kikubwa na kuzalisha bidhaa zenye ubora ambapo kwa kipindi kilichopira mapato yaliongezek kutokana na mauzo kwa silimia 3 na kufika Sh bilioni 221 kutokana Sh bilioni 215 kwa mwaka 2018.

Alisema mbali ya kupata faida hizo, kuna changamoto mbalimbali ikiwemo tya ongezeko la matarajio ya hasara iliyotokana na madeni kwa asilimia 22 kutoka Sh milionbi 305 kwa mwalka 2018 hadi Sh milioni 990  mwaka jana.

Alisema  kampuni iliwekeza kwenye gharama za mara moja za mauzo ambazo zilichangia  ongezeko la gharama za mauzo kwa silimia 19, ikilinganishwa na mwaka uliopita na kuongeza kuboresha mauzo, upelekaji bidhaa kwa wateja kwa kipindi kirefu.

“Wakurugenzi na viongozi wanayo imani  maamuzi haya yatalea matokeo chanya katika kipindi kifudi na cha kati hata hivyo kampuni haikutangaza gawio la muda mdfupi wala la muda mrefu kwa wanahisa kwa mwaka 2019 na mwaka 2018 kwa mtawalia sambamba na utendaji wake wa kifedha kwa mwaka.

“Bodi imeamua kuwa na biusara kwa kuweka rasilimali ya fedha iliyopo kwenye uendeshaji na kwa ajili ya kuwajibika katika kuhudumia deni. Bodi itakagua utendaji wa kigtedga kwa mwaka wa fedha 2020 wakati wa kutaka kyuia tamko la gawio

Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Tanga Cement,Reinhardt Swart alisema kufufuliwa tena kwa Shirika la Reli  Tanzania (TRC) kutoka Tanga kwenda mikoa  Arusha na  Kilimanjaro  kumesaidia kuongeza usambazaji wa saruji na kupunguza gharama kubwa walizokuwa wakizipata.

Alisema kampuni  imeweka mikakati dhabiti kuhakikisha kuwa uzalishaji unafika kila mahala Tanzania ikiwa ni pamoja na utoaji faida kwa wananchi kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo na hata wananchi wanaozungukwa na kiwanda hicho.

Alisema sababu za ongezeko la bei ya bidhaa zao  kutokana na ongezeko la gharama za uzalishaji, ongezeko la gharama za manunuzi ya makaa ya mawe, ongezeko la gharama za wafanya kazi na gharama za ukarabati wa mitambo ya uzalishaji saruji

“Kutokana na ongezeko la gharama za uzalishaji wa bidhaa zetu, kuna mpango wa kuongeza bei ya ifikapo mwezi Januari mwakani. Kabla ya ongezeko lolote la bei ni lazima wanahisa wetu wajue na kuridhia. Bei za bidhaa zetu zitaongeka bei kutokana na ongezeko la gharama za uzalishaji,” alisema.

Hata hivyo, Swart alisema kuwa licha ya uwepo wa sakata la ongezeko la bei ya saruji nchini,Tanga Cement PLC haijaongeza bei toka Juni, mwaka huu, nakuwanyooshea vidole wasambazaji wa saruji nchini kuwa ndio chanzo cha bei kupanda.

“Nadhani ni vema tukianganzia wanunuzi wa saruji kwa bei ya rejareja…Hapa tuna aina mbili za uuzaji wa saruji nchini; uuzaji wa saruji wa rejareja unaofanyika moja kwa moja, na pia kumuuzia mteja saruji kulingana na hitaji lake huku njia nyingine ikiwa ni kwa mteja kujaziwa saruji kwenye malori,”alisema.

Alisema Tanzania ina saruji ya kutosha kuwezesha sekta ya ujenzi kuchanua na haitawezekana ghafla tu kukawa na upungufu wa bidhaa hiyo.

Akizungumzia kuhusu uzaji wa saruji nje ya nchi,  alikiri wasambazaji wa saruji kuuza bidhaa hiyo nchini Rwanda na Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles