26.6 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Siku tatu za JPM Dar

Na MWANDISHI WETU – DAR ES SALAAM

ZIKIWA zimebaki siku 16 Watanzania kwenda kwenye vituo vya kura kwa ajili ya kuchagua Rais, wabunge na madiwani, mgombea urais kupitia CCM, Rais Magufuli anaanza mikutano mitatu mihumu katika Jiji la Dar es Salaam, akitarajiwa kufanya mikutano katika majimbo ya Segerea, Ubungo na Kawe.

Mikutano hiyo itafanyika kwa siku tatu mfululizo kuanzia leo Jumatatu, kesho na kesho kutwa, akirejea rasmi kwenye kampeni kwa mchuano wa mwisho ikiwa ni lala salama ya kampeni hizo.

Rais Magufuli anarejea kwenye kampeni baada ya mapumziko mafupi huku mpinzani wake mkuu anayewania urais kupitia Chadema, Tundu Lissu akiwa amerejea katika kampeni kwa kishindo, badaa ya mapumziko ya siku saba.

Wakati mgombea wa CCM, Rais Magufuli akiwa memaliza mapumziko ya siku nane kwa ajili ya kuweka mikakati ya chama chake na kushiriki shughyuli nyingine za Serikali, mgombea urais wa Chadema, Lissu alikuwa katika mapumziko ya siku saba baada ya kupewa adhabu na Kamati ya Maadili ya Uchaguzi kwa kile kilichodaiwa ni malalamiko yaliyowasilishwa na CCM na NRA kakidaiwa kusema uongo katika kampeni.

Ijumaa, mgombea wa CCM, Rais Magufuli alirejea kwa kishindo kwenye kampeni akianzia katika Jiji la Dar es Salaam ambao alinadi sera na maini yake kwa Watanzania.

Rais Magufuli alirejea tena kwenye majukwaa ya kampeni baada ya kuwa na mapumziko mafupi na sasa anaingia ngwe ya lala salama katika kampeni zake akiwa ameanzia katika Uwanja wa Taifa ambao sasa unajulikana kama Uwanja wa Mkapa ulioko eneo la Temeke, ametenga muda wa siku tatu kuanzia leo kuzunguka katika maeneo ya Dar es Salaam kunadi sera zake.

Kuanzia leo, Rais Magufuli atafanya mikutano ya kampeni katika majimbo matatu ya Dar es Salaam akijikita kueleza mafanikio ya utekelezaji Ilani ya 2015 – 2020 na yale yatakayotekelezwa miaka mitano ijayo

Mikutano hiyo itakayoanza leo hadi kesho kutwa itafanyika katika majimbo ya Segerea, Ubungo na Kawe.

KAMPENI: Mgombea mwenza urais kwa tiketi ya CCM Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na wananchii wa Jimbo

la Kwela alipowasili katika Kijiji cha Kalakala Sumbawanga Vijijini mkoani Rukwa kwa ajili mkutano wa kampeni jana.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole, alisema mkutano mkubwa utafanyika katika Jimbo la Segerea eneo la Kinyerezi mwisho leo (Njia panda ya kwenda mitambo ya kufua umeme wa gesi).

Aidha alisema kesho Jumanne mkutano utafanyika Jimbo la Ubungo eneo la Mburahati uwanja wa Barafu na kwamba kesho kutwa mkutano mkubwa wa kufunga kampeni katika Jiji la Dar es Salaam utafanyika Jimbo la Kawe viwanja vya Tanganyika Packers.

Polepole aliwaomba wana CCM na wananchi wote kwa ujumla kujitokeza katika mikutano hiyo itakayoanza kuanzia saa 2 asubuhi.

“Mikutano yote mitatu ratiba yake ina sehemu mbili, sehemu ya kwanza ni maelezo ya utekelezaji Ilani ya 2015 – 2020 kutoka kwa wagombea ubunge wa CCM sambamba na kuomba kura na sehemu hii inashereheshwa na vijana wa CCM, wasanii wa muziki ambao pia watayaeleza mafanikio ya awamu ya tano kwa lugha ya sanaa.

“Sehemu ya pili itaelezwa na ndugu Magufuli ambaye ataeleza tulikotoka, tuliko na tunakokwenda, itakuwa fursa ya kuyasikia maono yake kwa Dar es Salaam na taifa,” alisema Polepole.

Wiki iliyopita wakati wa mkutano uliofanyika uwanja wa Benjamin Mkapa, Dk. Magufuli alisema Jiji la Dar es Salaam ni muhimu kwa sababu lina idadi kubwa ya watu na limekuwa likiongoza kwa kuchangia katika Pato la Taifa kila mwaka kwani asilimia 90 ya mapato hasa ya kodi yanatoka katika jiji hilo.

Kwa mujibu wa Dk. Magufuli kwa sasa jili hilo lina wakazi milioni sita na itakapofika mwaka 2030 idadi hiyo inakadiriwa kuongezeka na kufikia milioni 10.

Alisema mwaka 2015/16 mapato ya jiji hilo yalikuwa Sh trilioni 11.9, 2016/17 (Sh trilioni 12.6), 2017/18 (Sh trilioni 13.6), 2018/19 (Sh trilioni 13.9), 2019/20 (Sh trilioni 16.01).

“Kwa miaka mitano Dar es Salaam imeendelea kuongoza kuchangia Pato la Taifa hii inadhihirisha umuhimu wa jiji hili kwa maendeleo ya nchi yetu. Jiji hili ni lango kuu la shughuli za uchukuzi na usafirishaji kwa sababu nchi yetu inapakana na nchi nane na kati ya hizo sita zinategemea bandari ya Dar es Salaam kupitisha mizigo yao,” alisema Dk. Magufuli.

Dk. Magufuli alisema anazifahamu kero mbalimbali katika kila wilaya ya jiji hilo na kuwaomba

wananchi wamwamini kwani amejipanga kufanya maajabu.

“Bado nina moto mkali na Dar es Salaam kwa ajili ya kuwaletea maendeleo, nataka watu watakapokuwa wanateremka Dar es Salaam wajue wapo Ulaya,” alisema.

Dar es Salaam unakuwa mkoa wa 14 kufanya kampeni tangu chama hicho kilipozindua kampeni zake Agosti 29 jijini Dodoma.

Mikoa mingine ambayo Dk. Magufuli ameshafanya kampeni ni Singida, Tabora, Shinyanga, Simiyu, Mwanza, Mara, Geita, Kagera, Kigoma, Njombe, Iringa, Mbeya na Songwe.

GAWIO LA BARRICK

Katika hatua nyingine Polepole alisema kesho pia Rais Magufuli atawaongoza Watanzania kupokea mgawo wa zaidi ya Sh bilioni 100 kutoka Kampuni ya Barrick Gold ikiwa ni sehemu ya mafanikio ya kupitia upya mikataba ya madini na kutunga sheria za madini na zinazolinda maliasili hapa nchini.

Wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika mwanzoni mwa mwezi uliopita katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, Dk. Magufuli alifafanua kuwa kutokana na ubia baina ya Serikali na Barick uliowezesha kuundwa kwa Kampuni ya Twiga, serikali itapata faida ya zaidi ya Sh bilioni 230.

Alisema Sh bilioni 23 zitaelekezwa kuimarisha uwezo wa mitambo ya serikali, Sh bilioni 11.5 (mchango wa kuimarisha uwezo wa kuhifadhi madini), Sh bilioni 23 (zitatolewa kwa vyuo vikuu kuendeleza na kuimarisha mafunzo ya wataalam), Sh bilioni 92 (kuimarisha barabara za lami hadi mgodi wa Bulyanhulu, Sh bilioni 62.514 (mfuko wa maendeleo).

Alisema pia makao makuu ya kampuni hiyo yatakuwa jijini Mwanza.

LISSU ACHANJA MBUGA

Kw aupande wake, mgombea urais wa Chadema, Lissu ameendelea kuchanja mbuga baada ya kurejea kwenye kampeni akianzi mjaini Dodoma juzi, mji muhimu ambao ndio makanomakuu ya nchi kwa sasa

Kwa mujibu wa ratiba ya NEC, baada ya kutoka Dodoma juzi, jana Lissu anaendelea na mikutano yake Singida, kisha atakwenda Tabora, Shinyanga , Geita, Mwanza, Mara, kisha Tabora, Singida na kurudi Dodoma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles