26.1 C
Dar es Salaam
Friday, December 9, 2022

Contact us: [email protected]

Daktari atoa sababu wanaume kuongoza magonjwa ya akili

Na AVELINE KITOMARY – DAR ES SALAAM

MWENYEKITI wa Chama cha wataalamu wa afya ya akili Tanzania, Isaack Lema amesema kuwa sababu ya idadi kubwa ya wanaume kukubwa na magonjwa ya akili kuliko wanawake inatokana na tabia ya kutokuzungumza au kulia pindi wanapokumbana na matatizo.

Kwa mujibuw a taakwimu zilizotolewa na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili mwaka 2018/19, idadi ya wanaume wanaougua ugonjw awa akili ni 18,535 huku wanawake wakiwa ni 10,631.

Akizungumza na MTANZANIA katika mahonjiano maalum jijini Dar es Salaam Lema ambaye pia ni Msaikolojia Tiba katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alisema sababu zingine ni mtoto wa kiume kusahaulika katika malezi na uwezeshwaji.

“Zipo sababu nyingi na hapa tunaagalia magonjwa yanayopatikana kwa kiwango kikubwa katika jamii ni pamoja na magonjwa ya sonona,magonjwa ya hisia (bypola), skizofeni na magonjwa ya matumizi ya vilevi .

“Sasa tukiangalia haya magonjwa makubwa mfano sonona mara nyingi pia sasa wanaume wanaonekana kuwa na dalili au viashiria vya ugonjwa huu na sababu kubwa ni wanaume hawaongei mambo yao hata wanapokubwa na matatizo hukaa kimya au mara nyingi unakuta wanaendana katika njia ambazo sio za kiafya na hizo njia ni matumizi ya vilevi .

“Ukiangalia kundi kubwa la wanaume wamejiingiza kwenye matumizi ya vilevi kama pombe,bangi na dawa za kulevya na kutokana na kujiingiza kwingi vilevi vinaathiri ule mfumo wa akili uliopo kwenye mwili wa binadamu na kupelekea mchocheo na mwamko wa magonjwa ya akili,”alibainisha.

Alisema matumizi ya vilevi yanachangi wanaume kukumbana na magonjwa ya akili

“Lakini pia kuna magonjwa ambayo dalili yake mmoja wapo ni mtu kusitisha uhai wake ukiangalia vitu wanavyotumia wanaume kusitisha uhai wao unakuta mara nyingi huwa ni vigumu kwa upande wa wanawake ,Kwahiyo anaweza kutumia mbinu ambazo zinaweza kukamilisha tatizo,”alieleza Lema.

Kumsahau kijana wa kiume ni moja wapo ya sababu ambazo zinachangia wanaume kukumbana na magonjwa ya akili kwa kiwango kikubwa kuliko wanawake.

Lema alisema ni muhimu sasa jamii kushtuka katika hili ili kuokoa afya na maisha ya vijana wa kiume.

“Malezi ya mabinti yamebadilika kwa kipindi kirefu kumekuwa na kitu cha kumjengea uwezo binti na wanawake lakini ni nani anayewajengea uwezo vijana wa kiume ,ni nani anawajengea uwezo wa kuweza kuendelea kuyaona ni yapi yanafaa?aliuliza.

Aliongeza “Mfumo uliobaki ni wakuonesha wanaume ni jasiri, ni mtu ambaye anatakiwa kuwa mkakamavu anaweza kuhimili yote lakini na yeye ni binadamu ,kwahiyo leo hii ukimruhusu mwanaume alie inaonekana kama umeruhusu udhaifu lakini naye ni binadamu anahisia kama wengine.

“ Kwahiyo ninachosema ni kwamba kumsahau mtoto wa kiume katika malezi na kumsaidia kumjengea uwezo baadaye ni changamoto pia hii husababisha wanaume kuwa kwenye matatizo.

NINI KIFANYIKE?

Lema alisema kwasasa wanaendelea kuhamasisha wanaume wazungumze kuhusu matatizo wanayopitia.

“Wanaume tunazungumza kwa namna gani kuna vile vikao vya kiume ,vikao vya baba na kijana wake ,kaka na mdogo hivi vikao tuzungumze kuelezea hisia zetu na wakati mwingine sio tu kuonesha uwezo tulionao lakini pia namna gani tunaweza kupambana na madhaifu yaliyopo.

“Ukiacha kuongea kitu kingine wanaume pia tusitumie vilevi kama sehemu mmoja wapo ya kuendana na maisha tunavyokabiliwa na changamoto tutafute maarifa ya kutatua kuliko kujiingiza kwenye kujiendana na matatizo kwa njia ya vilevi.

“Lakini kingine ninachoweza kusema ni vizuri wanaume wakajengewa uwezo wa kuhimili changamoto za sasa kwasababu changamoto wanazokutana na wanaume wa sasa ni tofauti na zamani nasema hivyo kwasababu mwanamke amewezeshwa yuko juu sasa na anakipato,”alieiza Lema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,734FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles