30.6 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Msalaba Mwekundu kutoa elimu ya corona

Na YOHANA PAUL

SHIRIKA la Msalaba Mwekundu Mkoa wa Mwanza limeanzisha kampeni ya utoaji elimu ya kujikinga na virusi vya corona katika wilaya zote na maeneo ya mjini na vijijini ili kuhakikisha athari za maambukizi ya virusi hivyo haizidi kuwa kubwa nchini.

Akizungumuza na waandishi wa habari, Mratibu wa Red-Cross Mwanza, Salome Tuppa, alisema kwa kutumia nafasi waliyonayo kama shirika, wameamua kubeba majukumu ya kueneza elimu hiyo Mkoa wa Mwanza ili kuendelea kuufanya kubaki salama dhidi ya athari ya virusi vya corona.

Tuppa alisema katika utoaji wa elimu hiyo watawekeza zaidi katika kusambaza vipeperushi vyenye elimu ya kujikinga na corona vilivyoandaliwa na Wizara ya Afya na kuweka mabango makubwa kwa maeneo yote ili kila mwananchi achukue tahadhari ya janga hilo.

“Katika kufanikisha elimu hii inamfikia kila mtu, tumepanga kupita wilaya zote za Mkoa wa mwanza na kuhakikisha wananchi wote walio maeneo ya mjini na vijijini wanapata elimu hii kwani kwa maeneo ambayo yapo mbali zaidi tutatumia hata madereva bodaboda kusambaza vipeperushi na mabango ya elimu ya corona,” alisema Tuppa.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dk. Thomas Rutachunzibwa, alisema shirika hilo limepewa jukumu la kueneza elimu ya kujikinga na corona Mkoa wa Mwanza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles