29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 30, 2024

Contact us: [email protected]

Upepelezi kesi ya kina Kitilya bado haujakamilika

PATRICIA KIMELEMETA –Dar es salaam

ALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya  Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya na wenzake wanaendelea kusota mahabusu kutokana na upelelezi wa kesi yao kutokamilika hadi sasa.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni pamoja na waliokuwa maofisa waandamizi wa Benki ya Stanbic, Sioi Solomon na Miss Tanzania mwaka 1996, Shose Sinare.

Wakili wa Serikali, Mwanaamina Kombakono, aliieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam mbele ya Hakimu Mkazi Janeth Mtega kuwa kesi hiyo ilipangwa kutajwa juzi, lakini upelelezi wake bado haujakamilika na kuomba tarehe nyingine.

Baada ya kusikiliza maelezo hayo, Hakimu Mtega, aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 11, mwakani.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kutakatisha fedha na wanaendelea kusota rumande kwa takribani miaka miwili sasa kutokana na upelelezi kutokamilika.

Wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Machi 2013 na Septemba 2015 wakati wa mchakato wa mkopo wa Dola za Marekani milioni 550 kwa Serikali ya Tanzania kutoka Benki ya Standard ya Uingereza.

Wanadaiwa kuwa Machi 2013 jijini Dar es Salaam walijipatia Dola za Marekani milioni sita, wakionesha kuwa fedha hizo zilikuwa ni malipo ya ada ya uwezeshaji upatikanaji wa mkopo na zililipwa kupitia  Kampuni ya Egma Tanzania Ltd.

Washtakiwa hao wanadaiwa kutakatisha fedha kwa kuhamisha, kuchukua na kuweka kiasi cha dola milioni sita katika akaunti tofauti za benki.

Kati ya Machi 2013 na Septemba 2015, wanadaiwa kuwa waliweka fedha hizo katika akaunti mbalimbali zilizomilikiwa na Kampuni ya Egma na walipaswa kufahamu zilikuwa ni mazao ya uhalifu wa kughushi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles