33.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 29, 2024

Contact us: [email protected]

LOWASSA: MONDULI MSIFE MOYO

|Mwandishi Wetu, Dar es Salaam



Muda mchache baada ya Mbunge wa Monduli, Julius Kalanga (Chadema), kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, amewataka wananchi jimboni humo wasife moyo na kuwa na utulivu.

Lowassa ambaye pia amewahi kuwa Mbunge wa Monduli kabla ya Kalanga, amesema amesikia taarifa za kujiuzulu kwa mbunge huyo na kwamba kwa sababu zozote ambazo amezitoa ni haki yake kikatiba.

“Najua Wana-Monduli wote nikiwamo mimi uamuzi huo umetuhuzunisha na kutuumiza, lakini nawaomba msife moyo hata dakika moja zaidi kitendo hicho kizidi kutupa nguvu, ari, hamasa na mori zaidi ya kuendeleza mapambano ya kuitafuta demokrasia na mabadiliko ya kweli.

“Hakuna jipya katika hili, ni kawaida kwa wanasiasa duniani kuhama vyama vyao na kubadilishana vijiti. Monduli imetupa heshima kwenye harakati za mabadiliko, naomba msife moyo,” amenukuliwa Lowassa ambaye pia ni Mjumbe Kamati Kuu ya Chadema.

Taarifa za Kalanga kutaka kukihama chama hicho, zilianza kusambaa jana zikidai angetangaza uamuzi huo leo, hata hivyo alipoongea na Mtanzania Digital jana usiku alikanusha taarifa hizo akidai uzushi lakini saa moja baadaye mbunge huyo alitangaza kujiondoa chadema na kuhamia CCM.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles