22.2 C
Dar es Salaam
Saturday, October 1, 2022

LUGOLA, ZITTO HAPATOSHI

NIMEKUJA: Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza Dar es Salaam jana baada ya mfanyabiashara Said Lugumi (kulia) kuitikia wito wa kufika wizani hapo jana.Katikati Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Ramadhan Kailima. PICHA SILVAN KIWALE

DOROTH MNUBI NA LEONARD MANG’OHA-DAR ES SALAAM                |      


WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amemtaka Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe, kujisalimisha kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, vinginevyo atamwagiza Kamanda wa Polisi nchini, IGP Simon Sirro, kumkamata popote alipo.

Wakati Lugola akitoa agizo hilo, Zitto amesema hawezi kutii wito wa mwanasiasa na kama polisi wanamtaka watoe wito wa kisheria atakwenda.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Lugola alisema ndani ya siku mbili anataka mbunge huyo kufika kwa RPC Lindi.

Alisema mbunge huyo alitumia lugha ya matusi dhidi ya viongozi na amekiuka agizo la rais la wanasiasa kutofanya mikutano nje ya maeneo yao.

Pia Lugola amemwagiza IGP Sirro kuchukua hatua dhidi ya Mkuu wa Polisi (OCD) Wilaya ya Kilwa kwa kutomchukulia hatua Zitto kwa kutenda kosa katika eneo lake.

“Nina mambo mawili, moja ni baadhi ya Watanzania wenzetu ambao bado wanajihusisha na mambo ya kutoa kauli za uchochezi na kutukana viongozi, lakini pia bado wanakaidi agizo la Rais Dk. John Magufuli, hasa wabunge kutoka maeneo ya majimbo yao na kwenda kufanya mikutano kwenye majimbo yasiyo ya kwao.

“Na wanapofika kwenye majimbo ambayo si ya kwao, wanajihusisha na kutukana viongozi na kutoa lugha za kichochezi. Nataka niwaambieni Watanzania nimekwisha kemea jambo hili na nimesema chaguzi zote zinazoendelea hivi karibuni na zitakazoendelea mwakani na milele, nimesema hakuna ambaye atapona kama ataendelea kutukana viongozi na kutoa lugha za uchochezi.

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,373FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles