30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

GOODLUCK GOZBERT ALISHWA MAPERA KAMBI YA JESHI

NA CHRISTOPHER MSEKENA

STAA wa muziki wa Injili nchini, Goodluck Gozbert amesema moja ya jambo ambalo hawezi kulisahau kwenye maisha yake ni kupewa adhabu ya kula mapera mti mzima baada ya yeye na wenzake kukatisha kwenye kambi ya jeshi Nyamanoro jijini Mwanza na kuanza kula matunda hayo bila ruhusa.

Akiungumza na Juma3tata, Goodluck alisema yeye na rafiki zake wawili walikuwa na tabia ya kusindikizana baada ya kutoka shule, siku hiyo walikuwa wametoka kumsindikiza mwenzao na kuamua kupita njia fupi inayokatika katikati ya kambi ambapo walikutana na miti ya mapera.

“Saa ya kurudi tukasema tupite ‘shortcut’ kwa sababu jeshini mchana  huwa wanarhusu kupita ila mwisho saa 12 jioni, wakati tunaingia tukaona miti ya mapera na njaa njaa zetu kila mtu akadandia mti wake na kuanza kula, ghafla akatokea mwanajeshi ambaye alikuwa amevaa kiraia,

“Akatuluuliza madogo mna njaa eeh? Mimi nikajibu sana bro, basi jamaa akapita zake, baada ya muda akarudi na wenzake wawili wakati huo sisi tulikuwa tunajipa moyo kuwa jeshini kuna watu wana roho nzuri maana tulidhani wanakaa wababe tu, cheki huyu jamaa katuuliza tuna njaa harafu katuacha,” anasema Goodluck.

Akaongezea kuwa kila mwanajeshi akasimama chini ya mti na kuwaamrisha wayale mapera yote yaliyopo juu ya mti kitendo ambacho kiliwatoa machozi yeye na wenzake.

“Nashukuru mti wangu ulikuwa na mapera machache, kwa hiyo nikala nikabakiza vidogo vidogo lakini wenzangu kila mmoja alikuwa analia kivyake, mwanajeshi mmoja akaniruhusu niondoke wakati nipo njiani tena nikakutana na mwanajeshi mwingine, akanirudisha kwa kuchurachura, mpaka baadaye tunaruhusiswa na wenzangu, wanajeshi wale wakatusindikiza hadi getini na kila mmoja akaelekea kwao bila kuongea na mwenzake,” alisema Goodluck Gozbert anayefanya vizuri hivi sasa na wimbo unaoitwa Shukurani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles