25.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 30, 2024

Contact us: [email protected]

KIKONGWE KORTINI AKIDAIWA KUTAPELI MILIONI 8/-

Na FARAJA MASINDE-DAR ES SALAAM

KIKONGWE Leopard Lucas (66), amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kujibu mashtaka 10 likiwemo la kutapeli.

Lucas anadaiwa kutapeli kiasi cha Sh milioni 8.9 baada ya kuwauzia watu 10 viwanja ambavyo ni mali ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA).

Akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi, Flora Mjaya, Wakili wa Serikali, Neema Mushi, alidai mshtakiwa anadaiwa kujipatia kiasi hicho cha fedha kwa njia ya udanganyifu.

Alidai katika shtaka la kwanza, mshtakiwa alitenda kosa hilo Agosti 28, 2010 katika eneo la Nyeburu Chanika ambapo alijipatia Sh 900,000 kutoka kwa Selemani Hamisi baada ya kudai kuwa atamuuzia eneo la ardhi wakati akijua eneo ni mali ya Mamlaka ya Viwanja vya ndege.

Hata hivyo, ilidaiwa mahakamani hapo kuwa eneo hilo alishalipwa fidia ya Sh 6,126,000 na TAA na kutakiwa kuondoka lakini yeye aliendelea kuuza eneo hilo kwa watu hao.

Mushi alidai shtaka la pili, Novemba 10, 2010, mshtakiwa alijipatia Sh 500,000 kutoka kwa Rukia Athumani, ili amuuzie eneo la ardhi wakati akijua kuwa eneo hilo si mali yake bali ni mali ya TAA.

Katika shtaka la tatu, Novemba 10, 2009, katika eneo hilo alijipatia Sh milioni 1.5 kutoka kwa Severina Mgaya, huku shtaka la nne mshtakiwa huyo akidaiwa alijipatia Sh 900,000 kutoka kwa Aminirabi Elimika kuwa atamuuzia kiwanja wakati akijua kuwa si kweli.            

Shtaka la tano, katika eneo hilo, Lucas alijipatia Sh 400,000 kutoka kwa Mary Ilalidi na shtaka la sita alijipatia Sh milioni 1 kutoka kwa Meshack Ndumbe kuwa atamuuzia kiwanja wakati akijua kuwa eneo hilo ni mali ya TAA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles