33.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

TETEMEKO LABOMOA MAJENGO, LAUA 100 INDONESIA

Waokoaji wakijaribu kuunasua mwili wa mwathirika wa jengo lililoporomoka baada ya tetemeko la ardhi kupiga katika Wilaya ya Pidie Jaya, Jimbo la Aceh, Indonesia jana.
Waokoaji wakijaribu kuunasua mwili wa mwathirika wa jengo lililoporomoka baada ya tetemeko la ardhi kupiga katika Wilaya ya Pidie Jaya, Jimbo la Aceh, Indonesia jana.

ACEH, INDONESIA

IDADI ya watu waliofariki kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea Mkoa wa Aceh, magharibi mwa Indonesia, imefikia 97 huku wengine zaidi ya 600 wakijeruhiwa.

Ofisa habari wa masuala ya dharura katika mkoa huo, Heni Nurmaini, amesema tetemeko hilo lenye ukubwa wa 6.4 katika kipimo cha richter, limeharibu nyumba zaidi ya 200, majengo ya maduka, shule, misikiti na mengine.

Meja Jenerali Tatang Sulaiman, alisema operesheni ya uokoaji inaendelea, na kwamba tayari askari jeshi 1,050, polisi 900 na maofisa kutoka mamlaka ya kusimamia matukio ya dharura wamepelekwa eneo la tukio.

Maofisa walisema watu wengi wamefukiwa kwenye vifusi vya majumba yaliyoporomoka.

Mwaka 2004, Mkoa wa Aceh uliathiriwa na kimbunga kilichosababishwa na tetemeko kubwa baharini, ambalo liliua watu 120,000.

Taasisi ya Jiolojia ya Marekani, imesema tetemeko hilo lilitokea karibu na pwani katika Kisiwa cha Sumatra saa tano asubuhi za hapa  katika kina cha kilomita 17.2 chini ya ardhi.

Naibu Mkuu wa Wilaya ya Pidie Jaya, eneo lililoathiriwa zaidi  tetemeko hilo, Said Mulyadi, alisema huenda idadi ya waliofariki ikaongezeka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles