22.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

TRUMP AKATAA NDEGE MPYA ZA AIR FORCE ONE

usaf-airforceone

WASHINGTON, MAREKANI

RAIS mteule wa Marekani, Donald Trump, amesema anataka kufuta ombi la ununuzi wa ndege mpya za Air Force One zinazotumiwa na marais wa taifa hilo.

Zikiwa zimebaki wiki sita kabla hajaingia madarakani, bilionea huyo wa majumba, aliandika katika akaunti yake ya Twitter: “Boeing wanaunda ndege mpya aina ya 747 Air Force One maalumu kwa marais siku zijazo, lakini gharama yake imezidi, zaidi ya dola bilioni nne. Futa oda hiyo!”

Serikali ya Marekani iliingia mkataba na Kampuni ya Boeing wa kuundwa kwa ndege mbili au zaidi za kubeba marais.

Ndege hizo zilitarajiwa kukamilika na kuanza kutumiwa mwaka 2024.

Hisa za kampuni hiyo ya ndege ya Boeing zilishuka kwa zaidi ya asilimia moja baada ya ujumbe huo wa Trump kwenye Twitter, ingawa zilijikwamua baadaye alasiri.

Trump hatarajii kutumia ndege hizo mpya, iwapo hatashinda katika uchaguzi wa muhula wa pili mwaka 2020.

Rais huyo mteule pia alitangaza juzi kwamba benki ya SoftBank ya Japan imekubali kuwekeza dola bilioni 50 nchini Marekani, hatua inayotarajiwa kuunda nafasi 50,000 mpya za ajira.

Trump alifichua mpango huo baada ya kukutana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa SoftBank, Masayoshi Son ofisini katika ofisi yake iliyopo ndani ya jumba lake la Trump Tower.

“Masa alisema hawangechukua uamuzi huu wa uwekezaji iwapo sisi (Trump) hatungeshinda uchaguzi!” Trump alidai katika mtandao huo wa jamii.

Trump kwa sasa anatumia ndege yake binafsi, lakini atakapokuwa rais atahitajika kutumia Air Force One, ambazo zimeimarishwa mifumo ya usalama, ulinzi na mawasiliano.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles