33.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

MWANAHABARI WA KENYA AWAFUNDA WAHARIRI

Katibu wa TEF, Neville Meena
Katibu wa TEF, Neville Meena

MAULI MUYENJWA-DAR ES SALAAM

WAHARIRI wa vyombo vya habari nchini wametajwa kuwa ni kundi la watu waoga katika kudai haki ya uhuru wa vyombo vya habari na kuepuka kutumiwa na wanasiasa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana katika Mkutano wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Mwanahabari Mpekuzi kutoka Kenya, Mohamed Ally ametoa angalizo kwa wahariri akiwataka kuepuka kutumiwa na wanasiasa.

Mohamed ambaye alikuwa mmoja wa wageni waalikwa katika mkutano huo, alisema kuwa anaona wahariri pamoja na wanahabari ni waoga kudai haki hiyo, kulinganisha na nchi nyingine kama Kenya.

Alisema inatakiwa waandishi na wananchi ambao ndio wanufaikaji au wahanga wa kazi inayofanywa na waandishi wa habari kushikamana na kukataa sheria ambazo zimepitishwa kwa lengo la kukandamiza uhuru wa habari.

“Mahali mlipo sasa katika kurekebisha sheria ya vyombo vya habari hata Kenya tulikuwepo kwenye mchakato huo miaka ya 1980, Wakenya ni tofauti na mataifa mengi kuhusu suala la uhuru wa habari,  walisimama kidete kupinga vifungu kandamizi mpaka ikakubalika,”alisema Ally.

Mwenyekiti wa TEF, Theophil Makunga alisema wamekutana kwa mara ya kwanza na wahariri wa vyombo vya habari ili kujadili sheria zilizopitishwa kabla ya kwenda kutengenezewa kanuni ili kushauriana mahali ambapo bado kunahaja ya kudai mabadiliko.

“Sheria hii kwa kiasi kikubwa ni afadhali kushinda ile ya zamani, kuna mambo mengi ya muhimu ambayo yapo na niwatoe hofu waandishi wa habari kwa yale ambayo yanaonekana kuwa na mapungufu bado kunanafasi ya kuyabadilisha wakati wa kuitengenezea kanuni zake,”alisema Makunga.

Kwa upande wake Katibu wa TEF, Neville Meena alisema lengo kubwa la kukutana katika mkutano huo ni kujadili na kuangalia mapungufu  ya sheria hiyo kimfumo wa nchi na sheria hiyo ili kushauriana marekebisho yapi yadaiwe hata kama sheria hiyo imepitishwa bungeni.

“Tunawapa matumaini waandishi kwa maana kumekuwa na maneno mengi hasa katika suala la kiwango cha elimu ambacho mwandishi anatakiwa kuwa nayo, wakati kanuni zikitungwa kunauwezekano mengi yakaonekana hayatekelezeki kwa hiyo hapa leo tunapitia kila kitu hata kama hatukutoa maoni yetu katika muswada, muhimu ni kujua hatima ya  huko tuendako,”alisema Meena.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles