30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

TABORA, KATAVI, RUKWA ZAONGOZA MAAMBUKIZI VVU

NA LUCAS RAPHAEL


dt_140626_hiv_blood_vial_800x600

MIKOA ya Tabora, Katavi na Rukwa imetajwa kuwa ni miongoni  mwa mikoa  10 inayoongoza kwa maambukizi  ya virusi vya ukimwi.

Hiyo ni  kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2011/2012 za Taasisi ya Mkapa.

Taarifa hiyo  iliyotlewa na Meneja Mradi wa TB na Ukimwi kutoka Taasisi ya Mkapa, Dkt. Happenes  Wilbroad     katika mafunzo ya siku moja  ya viongozi wa dini  yaliyofanyika   Nzega.

Alisema  mkoa unaoongoza kwa maambukizi ya VVU kati ya mikoa hiyo mitatu ni  Rukwa wenyeasilimia  6.2 ukifuatiwa na Katavi asilimia  5.2 na Tabora asilimia 5.1.

Dk. Wilbroad alisema Taasisi ya Mkapa  imeanza kuendesha  mafunzo ya kuhakikisha wananchi wanatambua na kuepuka maambukizi mapya.

Alisema    jitiahada mbalimbali za kudhibiti maambukizi  hayo zinapaswa kufanyika  kunusuru maisha ya  wakazi wa maeneo hayo.

Alitaja sababu zinazochangia   maambukizi kuwa ni pamoja na ndoa za utotoni, tohara za jadi na baadhi ya wananchi kutozingatia elimu ya Ukimwi   na kukithiri  imani potofu za ushirikina.

Wakizungumza  baada ya mafunzo hayo, baadhi ya viongozi wa dini walisema watahakikisha wanashirikiana na serikali kwa kutoa elimu kwa jamii  dhidi ya mapambano ya Ukimwi.

Mussa  kassimu, Sheikh  wa mjini  Nzega  alisema elimu waliyopewa na wataalamu wa mafunzo hayo inalenga maagizo ya imani zao za dini hasa katika kukemea jamii dhidi ya mambo maovu.

Mchungaji wa Kanisa la AICT, Isaya lyaka,   AICT  alisema vitabu vya dini vinasema kila mmoja awe mwaminifu kwa mwenziwe  waliofunga ndoa na   kwa wale ambao bado wanapaswa kusubiri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles