26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

WATUMISHI ARUSHA WASABABISHA HASARA MIL 838/- KWA KUDANGANYA KUSOMA

Na JANETH MUSHI


00tnar-im1000-the-arusha-hotel-1475-1

WATUMISHI 71 walioomba ruhusa   kwenda masomoni kutoka Halmashauri za  Arusha Vijijini na Meru    mkoani  Arusha, wamesababishia hasara ya zaidi ya Sh milioni 837.5 baada ya kubainika hawapo masomoni.

Kamati ya ulinzi na usalama wilayani Arumeru kwa kushirikiana na halmashauri hizo iliunda tume ndogo kujiridhisha kuwapo watumishi hao masomoni.

Iligundulika kuwa  watumishi 306 waliomba kwenda masomoni katika vyuo vikuu mbalimbali   nchini lakini  kati yao, 71  hawapo vyuoni.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani humo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Alexander Mnyeti, alisema  watumishi hao wameendelea kupokea mishahara huku wengine wakilipiwa masomo yao na serikali bila kuwapo vyuoni.

“Tumebaini wengine waliaga kwenda masomoni kuanzia 2011 ila kutokana na kutokufuatiliwa hawajarudi mpaka sasa na wanaendelea kupokea mishahara.

“Wengine tunasikia wanafanya kazi katika NGO’S za watu binafsi, wakuu wa vyuo wametoa ushirikiano mkubwa kwa tume hiyo,” alisema Mnyeti.

Alisema  katika Halmashauri ya Arusha Vijijini, hasara iliyosababishwa na watumishi hao ni zaidi ya Sh milioni 342 huku Halmashauri ya Meru ikipata hasara ya zaidi ya Sh milioni 495.

Aliwataka  watumishi waliopo vyuoni ila wataona majina yao kwenye orodha hiyo, ndani ya siku 10 watoe taarifa na kuthibitishwa na wakuu wa vyuo wanavyotoka.

“Tunawapa   siku 30 warudishe fedha hizo kwenye akaunti za waajiri wao ili fedha hizo zitumike katika shughuli nyingine za maendeleo.

“Walete risiti za malipo ya fedha hizo kabla serikali haijachukua hatua nyingine kwa sababu  hawapo vyuoni wala kazini.  Hivi  watu wanaifanya serikali shamba la bibi?” alisema.

Alitaja vyuo hivyo ambavyo watumishi hao wamebainika hawapo kuwa ni Vyuo vikuu vya Arush,a Makumira, Mount Meru na Chuo cha Ualimu Patandi.

Vingine ni vyuo vikuu vya Ruaha Catholic, Teofilo Kisanji,   SAUT Mbeya, Mzumbe, SUA, Jordan, SAUT Mwanza, Chuo cha Ualimu cha Eckernfodre Tanga, Sebstian Kolowa, Mwalimu Nyerere Memorial, Chuo kikuu Kampala International, Chuo cha Uhasibu.

Vingine ni vyuo vikuu vya Mwenge Catholic, Stephano Moshi na KCMC huku tume hiyo ikiwa bado haijenda katika Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM).

Mnyeti alisema  baada ya watumishi hao kurejesha fedha hizo, hatua nyingine za sheria zitachukuliwa dhidi yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles