24.9 C
Dar es Salaam
Sunday, April 21, 2024

Contact us: [email protected]

Jumia Travel yatoa tuzo kwa hoteli zinazofanya vizuri

ed5dc7a152b1027bf6fafa1c3903a98996991808

KAMPUNI inayoongoza kwa huduma za hoteli kwa njia ya mtandao barani Afrika, Jumia Travel, imetoa tuzo kwa hoteli na washirika wake kwa lengo la kuleta chachu katika matumizi ya huduma za hoteli mtandaoni.

Akizungumza wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo hizo, Meneja Mkazi wa Jumia Travel Tanzania,  Fatema Dharsee, alisema  tuzo hizo pia zitapanua wigo wa huduma kwa wateja.

“Tumejumuika hapa kuzitambua na kuzitunuku hoteli zinazotoa huduma nzuri pamoja na kupendwa na wateja wa ndani na nje ya nchi.

Mbali na sababu hizo, lakini kikubwa zaidi ni kwa hoteli hizi kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia kupitia mtandao wa intaneti ambao unawezesha huduma zao kufikiwa na mtu yeyote duniani,” alisema Dharsee.

Aidha, Dharsee alisema vipengele vya tuzo za Jumia Travel Tanzania vilivyokuwa vikiwaniwa ni pamoja na chaguo la wasafiri ambayo imetolewa kutokana na maoni ya wateja au wageni wengi walioitembelea hoteli iliyoonesha ushirikiano mkubwa.

Nyingine ni hoteli bora inayochipukia, ambayo imetolewa kutokana na juhudi na jitihada zilizooneshwa katika sekta nzima kwa ujumla. Hoteli iliyopokea maombi zaidi kutoka kwa wateja pamoja na mshirika bora katika biashara, ambayo ni mahsusi kwa kuwaunga mkono na mchango mkubwa katika biashara.

“Kufanikiwa kwa tuzo hizi kunatoa fursa kubwa ya maandalizi ya mwakani, lakini pia kufungua milango kwa wadau wengine kujumuika nasi katika kuhakikisha sekta hii nayo inakuwa na mchango mkubwa katika kutoa ajira na kuongeza pato la taifa kwa ujumla,” alisema.

Katika hafla hiyo, hoteli zilizojinyakulia tuzo hizo ni pamoja na Serena, ambayo ilitunukiwa tuzo ya Mshirika bora katika biashara; Tanzanite Executive Suites ilitunukiwa tuzo ya Chaguo bora la wasafiri; Amaan Bungalows ilitunukiwa tuzo ya Hoteli iliyoonesha ushirikiano mkubwa; Harbour View Suites ilitunukiwa tuzo ya Hoteli iliyopokea maombi zaidi kutoka kwa wateja na Slipway ambayo yenyewe ilitunukiwa tuzo ya Hoteli bora inayochipukia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles