26.1 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Hussein Bashe: Serikali iunde Tume ya kitaalamu ya kufanya mapitio makubwa ya mfumo wa elimu

bashe

Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe ameanzisha mkakati wa kuishawishi Serikali kuunda tume ya kitaalamu ya kufanya mapitio makubwa ya mfumo wa elimu.

Kwa mujibu wa Bashe, Mfumo wa elimu kwa muda mrefu umeonesha udhaifu katika usimamizi, uendeshaji, udhibiti na ugharimiaji tangu Taifa la Tanzania lilipo amua kufanya ugatuzi wa madaraka, uliopelekea sekta ya elimu kuendeshwa chini ya wizara tatu tofauti.

Anasisitiza kuwa ili kufanya mabadiliko katika Elimu, ni vyema watu waungane kuitaka Serikali kuunda tume ya kitaalamu ya kufanya mapitio makubwa ya mfumo mzima wa elimu inayotolewa Tanzania bara ili kwenda sambamba na kasi kubwa ya mabadiliko ya kiuchumi duniani.

Anaongeza kuwa bado mazingira ya watoto kujifunza ni duni pia bajeti shule ya msingi ni ndogo.

“Kwahiyo basi tuungane kwa pamoja KUSAINI NA KUSHARE ili kwamba serikali ituundie tume ya kitaalamu ya kufanya mapitio makubwa ya mfumo wa elimu inayotolewa Tanzania Bara ili kwenda sambamba na kasi kubwa ya mabadiliko ya kiuchumi duniani,” alisema Bashe

Mchakato huo ukishapata saini zinazohitajika, utapelekwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungno wa Tanzania, John Pombe Magufuli pia katika Bunge la Jamhuri ya Tanzania.


 

>Kutia saini mkakati huo tembelea https://www.change.org/p/tanzania-goverment-serikali-kuunda-tume-ya-kitaalamu-ya-kufanya-mapitio-makubwa-ya-mfumo-wa-elimu?recruiter=606357143

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles