26.6 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Selous yapoteza asilimia 90 ya tembo  

TemboNa Daudi Manongi

 HIFADHI ya Taifa ya Selous, imepoteza asilimia  90 ya tembo kutokana na ujangili uliokithiri.

Ripoti iliyotolewa na Mfuko wa Hifadhi ya Wanyamapori na Mazingira Duniani (WWF), Dar es Salaam jana, ilisema kama Serikali haitachukua hatua kali dhidi ya ujangili, ifikapo mwaka 2022, wanyama hao watatoweka.

Ripoti hiyo ilisema miaka ya nyuma Selous ilikuwa moja ya mbuga kubwa barani Afrika ikiwa na tembo 110,000, lakini kutokana na ujangili uliokithiri miaka 40 iliyopita, wamebaki 15,000.

“Kumekuwapo na mahitaji makubwa ya pembe za ndovu nchini China jambo ambalo limeonekana kuwa kichocheo kikubwa cha mauaji ya wanyama hao,” ilisema taarifa hiyo.

Ilisema kuwa mbuga ya Selous inaingiza dola za Marekani milioni 6 kwa mwaka, ikilinganishwa na sekta ya viwanda inayochangia dola bilioni 5 katika pato la taifa.

Kutokana na hali hiyo, Wizara ya Maliasili na Utalii, imeweka mikakati madhubuti ikiwemo kuunda kitengo cha intelijensia na kuanzisha kanda nane za doria za ushirikiano katika mifumo ya ikolojia ya mbuga hiyo.

Mwaka 2014 Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), liliiweka mbuga ya Selous katika urithi wa asili ulio hatarini kutoweka duniani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles