26.6 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Profesa Mbarawa atangaza kiama kwa wakandarasi   

Profesa-Makame-MbarawaNA BENJAMIN MASESE, MWANZA

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ametangaza kiama kwa wakandarasi nchini.

Amesema wajiandae kuburuzwa mahakamani na kufutiwa usajili wa wa miradi yao itakapobainika kutekelezwa chini ya kiwango.

Kauli hiyo aliitoa jijini Mwanza jana alipofungua mkutano wa mwaka wa Bodi ya Wakandarasi (CRB).

Alisema Serikali ya awamu ya tano haitamvumilia wala kucheka na mkandarasi atakayeshindwa kufanya kazi kwa ubora unaolingana na fedha zilizotolewa.

Profesa Mbarawa alisema kwa miaka mingi watumishi wa umma wamekuwa wakichezea fedha za walipakodi  wakati wa utekelezaji wa miradi mbalimbali huku ikijengwa chini ya kiwango.

“Naomba nitangaze wazi  mbele ya umma kupitia vyombo vya  habari. Sitaki kusikia jengo limejengwa lakini ndani ya muda wa miezi sita au miaka mitano lina nyufa.

“Nitaanza  na mkandarasi husika, anafuatia msimamizi wa mradi na mwisho nitamalizia kuwafukuza viongozi wote wa CRB.

“Naomba kazi ya kufuta kampuni ambazo zinashindwa kutimiza masharti ya miradi iendelee.

“Heri kuwa na wakandarasi 10 wenye kutimiza vigezo kuliko kuwa na orodha ndefu ambayo inafanya kazi kiujanja ujanja. Mimi sitakubali kufanya kazi na watu wasio wadilifu katika matumizi ya fedha, hili nasisitiza kweli kweli,”alisema.

 

Aeleza serikali ya JK                                              

Profesa Mbarawa aligusia hali ilivyokuwa katika serikali ya awamu ya nne ya Rais mstaafu, Jakaya Kikwete, alisema wakati serikali ya sasa ilipoingia madarakani ilikuta  miradi ya ujenzi ikiwa imesimama kutokana na ukosefu wa fedha.

Alisema Serikali ya Dk. Magufuli ilikuta wakandarasi wakiwa wanadai zaidi ya Sh bilioni 650 ambazo tayari zimelipwa na miradi inaendelea kutekelezwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles