30.6 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Ofisi ya Msajili yapata vifaa maalumu

Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana baada ya kupokea msaada wa vifaa maalumu vya kieletroniki kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP). Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa shirika hilo, Philippe Poinsot. Picha na Deus Mhagale.
Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana baada ya kupokea msaada wa vifaa maalumu vya kieletroniki kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP). Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa shirika hilo, Philippe Poinsot. Picha na Deus Mhagale.

GRACE SHITUNDU NA AZIZA MASOUD, DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), limekabidhi Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, vifaa maalumu vya kuhifadhi kumbukumbu jambo litakalovilazimu vyama kuwasilisha taarifa za ukweli.

UNDP kupitia Mradi wa Uwezeshaji Demokrasia (DEP), ilikabidhi vifaa hiyo vya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEKNOHAMA) jana na kusema vina thamani ya dola za Marekani 250,000 takribani sawa na Sh 400 milioni.

Mradi huo wenye thamani ya dola za Marekani milioni 500, unahusisha taasisi mbalimbali za serikali ikiwamo Tume ya Uchaguzi.

Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, akikabidhiwa vifaa hivyo, alisema vitasaidia kutunza taarifa mbalimbali za vyama zinazokusanywa katika mikoa mbalimbali nchini ambazo zitakuwa katika mfumo mmoja utakaorahishisha upatikanaji wake pindi zinapohitajika.

“Zoezi la kuhakiki taarifa za vyama vya siasa lilikuwa ni moja ya changamoto, hasa katika idadi ya wanachama, vifaa hivi vitasaidia kuwa na idadi sahihi bila udanganyifu,” alisema na kuongeza kuwa ofisi zotre za msajili nchini zitaunganishwa katika mtandao mmoja,” alisema Jaji Mutungi.

Alisema Watanzania wategemee mabadiliko ya utendaji kazi wa ofisi ya msajili kutokana na uwapo wa vifaa hivyo na mifumo mipya iliyofungwa katika ofisi ya msajili.

Awali akikabidhi vifaa hivyo Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Philippe Poinsot, alisema lengo la msaada huo ni kuahakikisha Tanzania inaendelea kukuza demokrasia na kuthamini mchango wa vyama vya siasa.

“Tunaamini ofisi ya msajili itafanya kazi kwa uhakika zaidi  baada ya kupata vifaa hivi, dhumuni letu ni kuongeza ubora na kujenga uwezo wa demokrasia nchini,” alisema Poinsot.

Alisema vitu walivyokabidhi ni pamoja kompyuta za mezani na mpakato (laptop), scanner, mashine ya  kuchapishia, mashine ya kudurufu (photocopy), simu za mkononi, tablets pamoja na mafunzo ya matumizi ya vitu hivyo kwa wafanyakazi wa ofisi ya msajili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles