28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 30, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania yapunguza vifo vitokanavyo na UKIMWI kwa asiliamia 50

*Matumizi ya ARV yafikia 95%

Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), George Simbachawene amesema vifo vitokanavyo na UKIMWI vimepungua kwa asilimia 50 kutoka vifo 64,000 mwaka 2010 hadi 32,000 mwaka 2020.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), George Simbachawene akihutubia katika hafla ya Harambee ya uchangishaji wa fedha za kupanda Mlima Kilimanjaro ili kuendeleza mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI mwaka 2022.

“Maambukizi mapya ya VVU kwa watu wazima (miaka 15 na zaidi) yameshuka kutoka 110,000 mwaka 2010 hadi 68,000 mwaka 2020; na Maambukizi mapya kutoka kwa Mama kwenda kwa Mtoto (Mother to child transmission) yameshuka kutoka 18% mwaka 2010 hadi 7% mwaka 2020,” amesema Simbachawene.

Simbachawene ameyasema hayo kwenye harambee ya uchangishaji wa fedha za kupanda Mlima Kilimanjaro ili kuendeleza mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI mwaka 2022.

Amesema matumizi ya dawa za kufubaza VVU (ARV) kwa WAVIU wanaojua hali zao za maambukizi yameongezeka kutoka 95% mwaka 2016 hadi 98% mwaka 2020.

Aidha, maambukizi mapya ya VVU kwa watu wazima (miaka 15 na zaidi) yameshuka kutoka 110,000 mwaka 2010 hadi 68,000 mwaka 2020.

“Serikali, tayari imetenga fedha Sh Bilioni 1.88 kwenye bajeti ya 2022/2023 ili iendelee kuchangia AIDS TRUST FUND,” amesema Simbachawene.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), George Simbachaweneakimpongeza Mwanafunzi, Hosea Patric Lema (aliyesimama) kwa kupata daraja la kwanza mchepuo wa PGM katika mtihani wa kidato cha sita, anayelelewa katika kituo cha Jimbo Rainbow. Serikali imeahidi kumpatia Mkopo wa elimu ya Juu.

Amefafanua kuwa serikali itaendelea kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa afua zinazotekelezwa za Mwitikio wa VVU na UKIMWI zinaleta tija kwa makundi mbalimbali katika jamii.

Amesema ili kufikia malengo haya pamoja na mengine katika kuishinda vita hii dhidi ya VVU na UKIMWI, kunahitaji nguvu ya pamoja kati ya serikali na wadau wengine, hususan sekta binafsi ili kupata rasilimali fedha ya kutosha.

 “Kili challenge inalenga kupunguza athari za kupungua kwa misaada ya wahisani na kuiwezesha nchi kuimarisha uwezo wa ndani kwa ajili ya kudhibiti UKIMWI,” amesema Simbachawene.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko, amesema kutakuwa na wapanda baiskeli 28 kuuzunguka Mlima Kilimanjarao na wapandaji mlima kwa mguu 24.

“Kwa muda wa miaka 20 zoezi hili limekuwa likifanywa na kuchangia kiasi cha dola za kimarekani million 7 zimekusaywa na zimesaidia sana katika makabilia kuendeleza mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI,” amesema Dk. Maboko.

Aidha, Dk. Maboko amesema fedha zinazopatikana katika harambee zitasaidia sana katika kuendeleza mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI.

“Tumeunda Kill Trust Fund, wajumbe wa bodi wanatoka upande (GGM) Geita Gold Mine na wengine wanatoka Tume ya Kudhibiti na Kupambana na UKIMWI, bodi imesaidia sana katika kuja na mikakati ya kufanya mara baada ya kukusanya Fedha,” amesema Dk. Maboko.

Akizungumzia harambee hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai, ameshukuru wadau wote walioshiriki kwa lango la kutafuta  fedha za muitikio wa VVU na UKIMWI.

Nimatumaini yangu kwamba ushirikiano huu utaendelea ili kufikia malengo ya sifuri tatu, kufikia mwaka 2030 ya kutokuwa na maambukizi mapya, unyanyapaa na vifo vitokanavyo na UKIMWI. Kushuka kwa maambukizi ya UKIMWI ni matokeo ya pamoja ya Wadau wa sekta ya Umma na Binafsi,” amesema.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), George Simbachawene amekabidhi bendera katika kwa vijana watakao zunguka mlima kwa baiskeli na wale watakaopanda mlima mpaka kileleni kwa muda wa siku saba kwa lengo la kutunisha fedha kwa ajili ya ili kuendeleza mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI mwaka 2022.

Naye Makamu  wa Rais wa Kampuni ya Mgodi wa Geita Gold Mine(GGM), Simon Shayo, amesema wamekuwa wakikusanya fedha zinazosaidia maeneo mabalimbali, baadhi ya taasisi zimeasisiwa kutokana na uwepo wa mfuko huo ikiwemo kituo cha kulelea Watoto yatima kilichoko mkoani Geita.

“Kituo kilianza na watoto 13 lakini sasa wamefikia zaidi ya 170 ambao wanapata elimu, huduma za afya kutokana na watu wanajitolea kuchangia kupitia mfuko. Kundi la kwanza la watoto walioingia kwenye kituo hicho wengi wao wako chuo kikuu,” amesema Shayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles