Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM
RAIS Dk. John Magufuli amemteua Adolf Ndunguru kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango anayeshughulikia Sera.
Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, ilieleza kwamba Ndunguru aliteuliwa kushika nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango (Sera) ambayo ilikuwa wazi.
Kabla ya uteuzi huo alikuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Kutokana na uteuzi huo Rais Magufuli amemteua Msafiri Mbibo kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa TRA.
Kabla ya uteuzi huo Mbibo alikuwa Meneja wa TRA Mkoa wa Kilimanjaro na taarifa hiyo ilieleza kwamba uteuzi wa viongozi hao ulianza janja Machi 31.