25.2 C
Dar es Salaam
Friday, August 12, 2022

JPM ateua Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha


Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

RAIS Dk. John Magufuli amemteua Adolf Ndunguru kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango anayeshughulikia Sera.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, ilieleza kwamba Ndunguru aliteuliwa kushika nafasi ya Naibu  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango (Sera) ambayo ilikuwa wazi.

Kabla ya uteuzi huo alikuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Kutokana na uteuzi huo Rais Magufuli amemteua Msafiri Mbibo kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa TRA.

Kabla ya uteuzi huo Mbibo alikuwa Meneja wa TRA Mkoa wa Kilimanjaro na  taarifa hiyo ilieleza kwamba uteuzi wa viongozi hao ulianza janja Machi 31.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,526FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles