27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 2, 2024

Contact us: [email protected]

WANA UFALME, MAWAZIRI WAKAMATWA SAUDI ARABIA

RIYADH,S AUDI ARABIA


MAMLAKA za Saudi Arabia zimewakamata wana ufalme 11, mawaziri wanne na matajiri wengi kwa tuhuma za kuhusika na rushwa.

Lakini pia hatua hiyo inadhaniwa ni mkakati wa mwanamfalme Mohammed Ben Salman (32) kudhibiti hatamu za uongozi.

Opereshini hiyo imekuja kipindi hiki ambacho Salman, mtoto wa kiume wa Mfalme Salman (81), anazidi kujirundikia madaraka na kufanya mageuzi ya kipekee katika sekta ya kiuchumi na kijamii katika nchi hii ya kihafidhina na kifalme.

Wimbi la kamata kamata linafuatia kuundwa tume mpya ya kupambana na rushwa inayoongozwa na Salman mwenyewe.

Miongoni mwa waliokamatwa ni pamoja na tajiri mkubwa, Al Walid Ben Tallal.

Zaidi ya hayo, mkuu wa kikosi chenye nguvu cha ulinzi wa taifa, Metab ben Abdallah, Mkuu wa Jeshi la Wanamaji, Abdallah Al-Sultani na Waziri wa Uchumi, Adel Fakih wameachishwa kazi ghafla.

Kwa mujibu wa Kituo cha Televisheni cha Al Arabiya, Tume ya Kupambana na Rushwa imeanzisha uchunguzi kuhusu kadhia ambazo baadhi zimetokea miaka mingi iliyopita.

Mwanasheria Mkuu wa Saud Arabia, Sheikh Saoud Al Mojeb, ambaye pia ni mjumbe wa tume hiyo, alisema watuhumiwa watapatiwa haki sawa na kutendewa sawa na raia yeyote wa Saud Arabia.

Muda mfupi baadae, Wizara ya Habari ikatangaza kufungwa akaunti za benki za wale wote waliokamatwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles