23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Bajeti ya Elimu yakita kwenye utafiti

kilangoNa Mauli Muyenjwa, Dar es Salaam
NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Anne Kilango amesema bajeti ya wizara hiyo ya mwaka wa fedha 2015/2016 inaongeza fungu kwa ajili ya utafiti.
Hayo aliyasema Dar es Salaam jana, alipofungua mkutano wa tatu wa wanasayansi mbalimbali nchini ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, (MUHAS).
Alisema sekta ya utafiti ni muhimu kwa ajili ya maendeleo ya taifa lolote duniani hivyo wizara yake imeona umuhimu wa kuiwezesha fedha ili kufanya utafiti wenye tija zaidi kwa taifa.
“Utafiti unahitajika sana na MUHAS ni wadau wakubwa katika suala hili, nawaahidi nitahakikisha kiwango cha bajeti katika utafiti kinaongezwa kukabiliana na changamoto zinazowakabili.
“Najua utafiti ni gharama lakini lazima tukubali kuwa bila utafiti hakuna kitu tunachoweza kufanya,” alisema.
Makamu Mkuu wa MUHAS, Profesa Ephata Kaaya, alisema utafiti unatakiwa kufanyika zaidi kubaini mbinu za kukabiliana na wimbi la ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza.
Alisema magonjwa yasiyoambukiza kama vile kisukari, shinikizo la damu na saratani, yamekuwa tishio na kuongezeka kwa kasi jambo ambalo ni hatari kwa taifa kwa vile linapoteza nguvu kazi ya vijana.
“Magonjwa haya zamani yalionekana kama vile yamesahaulika lakini sasa ni dhahiri kuwa hali ni mbaya hivyo tunatakiwa kuchukua hatua za haraka katika kukabiliana nayo kwa sababu watu wanaangamia kutokana na mtindo wa maisha kubadilika kwa kasi.
“Katika mkutano huu tunatarajia kujadiliana kwa kina namna ya kuzuia na hali ilivyo sasa tuweze kutambua wapi tuanze katika kukabiliana na hali hii,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles