26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

WHC yajivunia mafanikio ya miradi yake

FARAJA MASINDE – DAR ES SALAAM

Kampuni ya Nyumba ya Watumishi Housing (WHC) imewakaribisha wananchi hususan watumishi wa umma kutembelea kwenye banda lao katika maenyesho ya One stop jawabu ili kupata elimu namna wanavyoweza kupata makazi kwa gharama nafuu.

Wito huo Umetolewa leo na Afisa Uhusiano na Mauzo wa WHC, Maryjane Makawia wakati akizungumza na MTANZANIA kwenye maonyesho ya One Stop Jawabu yanayoendelea katika viwanja vya Zakheem, Mbagala jijini Dar es Salaam yakihusisha taasisi za serikali.

Amesema hadi sasa WHC inajivunia kwa namna ambavyo nyumba zao zimekuwa zikifanya vizuri ambapo kwa miradi ya Mwanza na Bunju B nyumba zimemalizika huku kwa Kigamboni nyumba za kununua zikisalia tatu.

“Tunawakaribisha watumishi mbalimbali wa umma ana wasio wa umma kuja kutembelea banda letu kwa ajili ya kupata taarifa kuhusu miradi yetu, ambayo imekuwa ikifanya vizuri katika kuwasaidia wananchi kuweza kumiliki makazi.

“Kwani kwa Dodoma nyumba za awamu ya kwanza pia zimeisha, pia kwasasa tunaendeleza ujenzi katika awamu ya pili, hivyo utaona kwamba tumeendelea kutengeneza mazingira rafiki kwa Watanzania kuweza kumiliki nyumba bora na za kisasa, kwani hata kwa wanaopanga kodi ni Sh 100,000 tu,” amesema Makawia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles