27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Wafanyabiashara Kagera watakiwa kufuatilia TIN

MWANDISHI WETU- KAGERA

MAMLAKA ya Mapato Mkoa wa Kagera (TRA) imewataka wafanyabiashara mkoani humo wenye vitambulisho vya ujasiliamali lakini wana vigezo vya kuwa na Namba za Utambulisho wa Mlipako (TIN) pamoja na kukadiriwa kodi kufika katika ofisi za mamlaka hiyo kwaajili ya kupatiwa TIN na kukadiriwa kodi.

Hayo yamezungumzwa jana mkoani hapa na Kaimu Meneja wa TRA Wilaya ya Muleba, Samwel Augustino baada ya kuzungumza na wafanyabiashara mbalimbali wakati wa kampeni ya Elimu ya Kodi ya mlango kwa mlango inayoendelea.

Alisema wamekutana na changamoto ya kukutana na wafanyabiashara ambao wanafanyabiashara lakini hawana TIN huku wengine wakiwa na vitambulisha vya ujasiliamali wakati wanavigezo vya kuwa na TIN pamoja na kukadiriwa kodi.

Alisema sambamba na changamoto hizo, changamoto nyingine waliyokutana nayo ni kwamba baadhi ya wafanyabiashara kumiliki TIN zisizo za biashara na wengine kumiliki TIN ambazo hazina biashara.

“Pamoja na changamoto lakini pia tumewakumbusha kulipa kodi ya awamu ya tatu mapemba ili kuepuka msongamano unaojitokeza katika siku za mwisho na kwamba tarehe ya mwisho ya kulipa kodi hiyo ni Septemba 30,”

Alisema katika kampeni hiyo inayoendelea mkoani Kagera, wafanyabiashara wanatakiwa kuitumia kampeni hiyo kwa kutoa ushirikiano wa maofisa wa TRA ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu kodi ikiwa ni pamoja na kuuliza maswali na kutoa maoni na changamoto zao wanazokutana nazo ili ziweze kutatuliwa.

Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Kata ya Nshamba Wilaya ya Muleba Leonidas Kitambi alisema kuwa anaipongeza TRA kwa kubuni mbinu rafiki ambazo zitawezesha kuongeza utayari wa wafanyabiashara kulipa kodi kwa hiyari.

Alisema hivi sasa wafanyabiashara wanafanya biashara zao kwa amani tofauti na ilivyokuwa zamani lakini kwa sasa TRA imekuwa ikitembelea katika maeneo ya wafanyabiashara na kutoa elimu mbalimbali ya kodi ikiwa ni pamoja na kusikiliza maoni na changamoto ambazo zimekuwa zikitafutiwa ufumbuzi.

Naye Fidelia Kalisa ambaye ni mfanyabiashara katika Kata ya Nshamba wilayani Muleba alisema kuwa kutokana na ugumu wa biashara uliopo sasa, mamlaka ya mapato ingefanya makadirio ya chini ya kodi ili waweze kumudu kuendelea kufanyabiashara zao.

Alisema zoezi linalofanywa na TRA la kuwatembelea katika biashara zao na kuwapa elimu ya kodi ni zuri na linatakiwa kuwa endelevu kwani litawasaidia kujua haki zao ikiwa ni pamoja na kujua umuhimu wa kulipa kodi kwa hiyari kwa maendeleo ya nchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles