22.4 C
Dar es Salaam
Friday, May 17, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Mkuu aagiza kuendelezwa kwa wataalamu wa michezo

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ziandae mkakati wa kuendeleza wataalam wa michezo, sanaa na burudani nchini.

“Miongoni mwa changamoto zinazoikumba sekta ya  michezo, sanaa na burudani ni eneo la kiufundi na mbinu. Hili linadhihirishwa na uwepo wa walimu wengi wa kigeni hususan kutoka baadhi ya nchi jirani kwenye mchezo wa soka,”.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumanne, Aprili 13, 2021) wakati akiwasilisha hotuba ya Mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka wa Fedha 2021/2022, Bungeni jijini Dodoma.

Majaliwa amesema licha ya kuendelea kukua kwa sekta ya sanaa, michezo na burudani nchini bado mchango wake katika uchumi ni mdogo. “Kwa mfano, tangu mwaka 2013 hadi mwaka 2019 sekta ya sanaa na burudani ilichangia asilimia 0.3 kwenye pato la Taifa,”.

Hata hivyo, Majaliwa amesema sekta hiyo inapata hamasa kubwa, inaajiri vijana wengi na kwa sasa na imekuwa miongoni mwa sekta zinazotumika kulitangaza Taifa nje na wakati mwingine kuvutia utalii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles