Mtibwa Sugar kuivaa Simba kivingine

0
344

Na Winfrida Mtoi, Dar es Salaam

Kaimu kocha wa timu ya Mtibwa Sugar, Soud Slim, amesema wataingia uwanjani kesho kucheza na Simba kwa mbinu tofauti na walivyocheza na Azam katika mchezo uliopita waliofungwa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Mtibwa inatarajia kucheza na Simba, mchezo wa kiporo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, saa 10:00 Alasiri kwenye Uwanja wa Mkapa,Dar es Salaam.
Kocha huyo amesema wamefanya maandalizi mazuri, licha ya kuwa watawakosa baadhi ya nyota wao ambao ni majeruhi akiwamo Salum Kihimbwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here