29.2 C
Dar es Salaam
Friday, May 17, 2024

Contact us: [email protected]

WAZAZI WALAUMIWA MIMBA ZA WANAFUNZI

Na DERICK MILTON



MKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Anderson Njiginywa amewalalamikia wazazi kuwa chanzo cha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kupata mimba wakiwa shuleni.

Wanafunzi 50 wameripotiwa kuwa na ujauzito kwa mwaka huu wilayani humo.
Njiginywa alisema hayo kwenye mahafali ya wanafunzi wa darasa la saba 41 na kidato cha nne 78, wa shule ya msingi na sekondari Simba wa Yuda wilayani humo.

Alisema viongozi wa vijiji, kata na halmashauri wamekuwa wakipata wakati mgumu kuwachukulia hatua wahusika wa wanaowapa mimba wanafunzi kutokana na wazazi kushindwa kutoa ushirikiano hatua hizo zichukuliwe.
“Wilaya ya Busega ni moja kati ya wilaya nchini zenye tatizo la mimba kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.
“Tumeshindwa kupambana na tatizo hilo kutokana na wazazi kuwa sehemu ya kuwalinda wahusika,” alisema Njiginywa.

Njiginywa alisema elimu kwa wazazi na wanafunzi inaendelea kutolewa pamoja na kuanzisha dawati la elimu hiyo katika kata mbalimbali wilayani humo.

Alisema hatua hiyo itaweza kupambana na tatizo hilo na aliwataka wahusika wakuu wa mimba hizo kuwa ni waendesha bodaboda na wavuvi kwa vile wilaya hiyo kupakana na ziwa Victoria.

Awali Mkurugenzi wa Shule hiyo, Josephales Mtebe, alisema nchi haina tatizo la kuwa na wasomi wengi, tatizo kubwa ni wasomi hao kutokuwa na hofu ya Mungu.

“Tatizo la watanzania ni kuwa na wasomi wengi wasiokuwa na hofu ya Mungu, kutokuwa na hofu ya Mungu kunasababisha kuwa na utendaji mbovu katika huduma za jamii.

“Ndiyo maana sisi Simba wa Yuda tunasema tunazalishaji viongozi wenye hofu na Mungu,” alisema.
baadhi ya wanafunzi waliohitimu shuleni hapo, Godluck William darasa la saba na Mariam Charles kidato cha nne, walisema matumaini yao ni kuendelea na masomo katika ngazi za juu zaidi kutokana na kuandaliwa vizuri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles