SERIKALI ya Zimbabwe imeweka wazi kuwa mtumishi wa umma ambaye atapuuzia na kutopata chanjo ya Corona hataruhusiwa kuingia ofisini.
Aidha, taarifa ya Serikali haijafafanya kama mtumishi asiyechanjwa atapoteza ajira au ataendelea majukumu yake ya kazi akiwa nyumbani.
Kwa mujibu wa Waziri wa Habari, Monica Mutsvangwa, Serikali imewapa muda watumishi kuhakikisha wanapata chanjo, kabla ya kuanza kusimamia utekelezaji wa agizo hilo.
Katika kile kilichoelezwa na Wizara, asilimia 90 ya wagonjwa walioko hospitali wakisumbuliwa na Covid ni wale waliopuuzia chanjo.
Kufikia sasa, Zimbabwe inatajwa kupokea maambukizi mapya 145 kila siku na jana viliripotiwa vifo saba.