31.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Chalamila:Tupo tayari kuwajibika ikibainika tulizembea na vifo hivi vikatokea

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema yeye na wenzake wapo tayari kuwajibika itakapoonekana walizembea kwa namna yoyote mpaka vifo vikatokea katika ajali ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa, Kariakoo iliyotokea Novemba 16,2024.

Chalamila ameyasema hayo leo Novemba 18,2024 kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam wakati wa kuaga miili 13 ya marehemu waliopoteza maisha katika ajali hiyo.

“Mimi pamoja na wenzangu, tumehisi tumefanya kazi mpaka pale tulipofikia na tunaendelea kufanya kazi. Ilitulazimu jengo hilo lisibomolewe bali tuanze kutumia akili kubwa kuliko nguvu ambayo ingeweza kupoteza watu wote.

“Mchakato huo Mheshimiwa Waziri Mkuu inawezekana kwa namna moja ama nyingine uliwakwaza watu wengi na kuona pengine hatujawajibika ipasavyo.
“Naomba Waziri Mkuu kwa kuwa wewe una vyombo vyako na kwa kuwa mchakato huu bado unaendelea,pale utakapobaini mimi au wenzangu hatukuwajibika kwa namna yoyote ile, tutakuwa tayari kuwajibika kwa sababu cheo nilichonacho si mali kuliko uhai wa watu.

“Tutakuwa tayari kuwajibika pale itakapoonekana tulizembea kwa namna moja ama nyingine mpaka vifo hivi vikatokea.

“Nayasema haya Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa sababu maneno yapokuwa pia ni mengi lazima sisi viongozi tuelimishane. Kwa kuwa ofisi yako ina upana wa taarifa na inafahamu mengi kutoka siku ya kwanza tukio hili lilipotokea,” ameeleza Chalamila.

Aidha amesema jitihada za kuwaokoa watu waliopo inaendelea na kuwashukuru wadau wote ambao walishirikia na ofisi yake kuokoa mali na watu, huku akisema usalama umeimarishwa katika eneo hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles